Thursday, September 26, 2013

WAREMBO WADAKWA WAKILEWA MUDA WA KAZI

Wakisubiri kusomewa…
Washitakiwa wakipelekwa kizimbani.
Afande akimlinda mmoja wa washitakiwa.
Wakisubiri kusomewa mashitaka.
WAREMBO wanne jana wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Sokoine Drive (Jiji) jijini Dar es Salaam kwa kosa la kunywa pombe za kienyeji muda wa kazi.
Warembo hao walinaswa maeneo ya Pugu nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Baada ya kufikishwa mahakamani hapo na kukana mashitaka hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, Timothy Lyon, aliwawekea wazi dhamana kwa kumtaka kila mmoja kuwa na wadhamini wawili na dhamana ya shilingi laki mbili kila mmoja. Sharti hilo la dhamana lilikuwa gumu kwa warembo hao ambao walipandishwa karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea mpaka tarehe 15 mwezi ujao.
                                                             PICHA : RICHARD BUKOS / GPL

No comments:

Post a Comment