Stori: Brighton Masalu
SHETANI anazidi kuiatamia dunia, ulimwengu unawayawaya! Jamaa mmoja
aliyetajwa kwa jina moja la Manfree, mkazi wa Kimara Mwisho, Dar ambaye
inadaiwa ni mfanyabiashara wa baa iliyopo Mbezi Mwisho (Mbezi Shamba)
anadaiwa kunaswa na mke wa mtu (jina tunalo), Risasi Mchanganyiko
linaibumburua.
Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lililoongeza faraja na furaha ya
shetani kule kuzimu, lilijiri juzikati huko Kimara Mwisho ndani ya gesti
moja (jina lipo kwenye droo zetu).
ALIYENASA AANZA KUMWAGIKA
Akizungumza kwa uchungu mkubwa, mume wa
mwanamke huyo ambaye hakupenda jina lake liupambe ukurasa huu, alisema
siku nyingi Manfree amekuwa akimsumbua mke wake, hali iliyokuwa ikimpa
wakati mgumu mwanamme huyo mwenye mke.
“Jamaa amekuwa akimsumbua
sana mke wangu, nilipokuja kuzipata taarifa hizi nilishangaa sana lakini
pia niliumia kama mwanamme,” alisema mwenye mke huyo.
MAZOEA YALIPOANZA
Kwa mujibu wa mume huyo, kufahamiana kwa
Manfree na mkewe kulikolea zaidi baada ya mwanamke huyo kuhitaji fremu
kwa ajili ya biashara ya duka ambapo kwa kutumia uenyeji wa jamaa huyo,
alionesha kutaka kumsaidia.
SINEMA YA KUNASWA ILIPOANZA
Mwanamme huyo aliendelea kusema kuwa
sinema ya kunaswa kwa mwanamme huyo ilianza siku moja baada ya yeye
kwenda kwenye baa ya jamaa huyo kuangalia mpira (hakuzitaja timu).
Alisema akiwa hapo baa, mara mke wake alitokea na kukaa kwenye kiti,
meza nyingine. Jamaa huyo naye akaenda kukaa na mke wa jamaa na kuanza
kuzungumza.
“Mimi sikujua walichokuwa wakikizungumza na wala sikuwa na wasiwasi
kwa vile jamaa ananifahamu, anafahamu yule ni mke wangu na anawafahamu
hadi watoto wangu,” alisema mwanamme huyo.
Akaongeza: “Tulipofika
nyumbani, mke wangu akasema amesikia mimi nina wanawake wengi nje,
nimewafungulia biashara na mambo mengine kibao.
“Nilimuuliza
ameambiwa na nani, akawa anagomagoma kunijibu lakini nilipombana sana
mwisho akamtaja jamaa. Kumbe alipokaa naye pale baa ndiyo alikuwa
akimwambia uongo huo.
“Mke
wangu akaongeza kusema kuwa jamaa huyo kwa muda mrefu amekuwa akimtaka
wakutane ‘praiveti’ lakini yeye amekuwa akimkatalia kwa sababu analinda
heshima ya ndoa yake.
“Mke wangu alinionesha meseji ambazo jamaa
alikuwa akimtumia, niliumia sana. Kwa kweli inauma sana jamani hasa
kitendo hicho kufanywa na mtu ambaye mnafahamiana!”
MTIRIRIKO UNAENDELEA
Kwa mujibu wa mwanamme huyo, hali hiyo iliendelea kuisumbua ndoa yake huku maneno ya Manfree yakizidi kumvuruga kichwani.
SINEMA KAMILI HII HAPA SASA
Mume huyo alizidi kueleza kuwa baada ya mkewe kukiri kwamba Manfree
amekuwa akimtaka wakutane chemba ndipo kwa pamoja walikubaliana kuandaa
fumanizi.
“Nilimwambia mke wangu lazima tutege fumanizi, lengo ni
kumfanya jamaa aachane na tabia hizi ambazo zinaweza kuharibu ndoa,
watoto wakateseka na mambo menginemengine. Nilimruhusu amkubalie
kukutana gesti,” alisema mume.
PICHA LINAKOLEA
Mume anasema siku ya tukio, Manfree bila kujijua
alimtumia meseji mwanamke huyo, akamuomba wakutane ndani ya gesti moja
iliyopo Kimara Mwisho ambapo bila kupoteza muda mwanamke huyo alimtonya
mumewe juu ya meseji hiyo.
“Baada ya kunionesha meseji hiyo nilitafuta baadhi ya marafiki zangu ili twende pamoja kwenye eneo la tukio wakawe mashahidi.”
UTAMU ZAIDI
Baada ya mke kufika ndani ya gesti hiyo, mume anadai alimtaarifu jamaa
huyo ambaye alitokea na kumwambia mwanamke huyo kuwa amuongezee shilingi
elfu kumi kwani chumba ni elfu ishirini.
CHUMBANI ZAIDI
Kwa mujibu wa mume huyo, baada ya wawili hao
kuingia chumbani humo, jamaa huyo alivua nguo zote na kukimbilia bafuni.
Nyuma, mwanamke huyo aliutumia mwanya huo kumtaarifu mumewe ambaye naye
aliwashika masikio marafiki ili wakae mkao wa kumnasa jamaa huyo.
Muda mfupi baadaye, mume anasema Manfree alitoka bafuni na kufikia
kitandani puu! Hana hili wala lile, mwanamme huyo akiwa na ‘skwadi’ yake
walizama ndani, wakagonga mlango, Manfree akakaribisha, alijua ni
mhudumu amemletea bia maana aliagiza.
Mume alizidi kusema kuwa jamaa
alipigwa butwaa na kuonekana kuweweseka. Yeye akamuuliza imekuaje yuko
na mke wake chumbani? Jamaa akawa hana la kujibu.
MAELEZO YA KWENYE VIDEO
Katika maelezo yaliyomo kwenye video ya tukio zima (ipo chumba cha
habari Global), Manfree anajieleza akimuomba msamaha mume huyo pamoja na
wote waliokuwa chumbani humo.
MKE WA MANFREE AITWA
Mwanaume huyo anadai kuwa kwa hasira aliamua
kumpigia simu mke wa Manfree ili afike kwenye gesti hiyo kushuhudia
mumewe alivyokutwa na mke wa mtu gesti.
Anasema: “Mke alifika, akamkuta mumewe hajavaa nguo, aliumia sana lakini hakuwa na la kufanya.”
JAMAA KIZIMBANI
Baada ya ‘mhangaikaji’ wetu kuzipata data hizo, juzi asubuhi alimtafuta
Manfree kwa njia ya simu ya mkononi kupitia namba alizopewa na watu wa
karibu. Mwanzoni jamaa huyo alionekana kugoma lakini baada ya kubanwa
kwa vielelezo alikubali huku akisema japo alinaswa lakini pia jamaa hao
walitumia njia za kumteka.
“Aa..! Ni kweli nilikutwa na zahama hiyo
lakini jamaa waliniteka bwana. Hata hivyo, sitarudia tena kuwa na
uhusiano na wake za watu na tulishamalizana na mwenye mke kwa kumuomba
msamaha,” alisema Manfree.
MKE WA MANFREE
Katika hali ya kushangaza, baada ya mkewe kupigiwa simu na mwandishi na
kukiri kuwa ni kweli mumewe alinaswa chumba cha gesti akiwa na mke wa
mtu, alisema bado anampenda na kwamba ndoa yao bado iko imara kama
mizizi ya mti wa mbuyu!
“Ni kweli mume wangu alifumaniwa lakini bado
nampenda sana na siwezi kumwacha, nitamvumilia maana ni mume wangu,”
alisema mke wa Manfree aliyejitambulisha kwa jina moja la Sarah.
(Maneno yaliyotumika kwenye picha za ukurasa wa mbele, ni kama wanasema na si maneno halisi.)
No comments:
Post a Comment