Sunday, May 19, 2013

YANGA v/s SIMBA ILIKUWA HIVI


Refa Martin Saanya kushoto akimdhibiti mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbangu asipigane na beki wa Simba SC, Nassor Masoud 'Chollo' kulia mbele ya kocha wake, Mfaransa, Patrick Liewig wakati wa mchezo wa kufunga pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taia, Dar es Salaam jioni ya leo. Katika tukio hilo, refa aliumia na kutibiwa kwa dakika tatu. Yanga ilishinda mabao 2-0. 

Wachezaji wa Yanga na Kombe lao baada ya mechi

Haruna Chanongo kushoto akimtoka David Luhende

Chanongo akikokota mpira pembeni ya Luhende

Luhende na Chollo

Abadallah Seseme akijaribu kupasua katikati ya Athumani Iddi 'Chuji' na Frank Domayo

Mbwembwe za Mrisho Ngassa leo

Frank Domayo anakwenda na mpira

Mwinyi Kazimoto akimtoka Kevin Yondan

Haruna Chanongo akitafuta mbinu za kuwatoka Nadir Haroub 'Cannavaro' na Mbuyu Twite

Mwinyi Kazimoto anakwenda

Athumani Iddi 'Chuji' akimiliki mpira mbele ya Amri Kiemba

Yanga na shangwe za ubingwa

Chuji na Kiemba...

11 walioanza Simba SC leo

11 walioanza Yanga SC leo

Wachezaji wa Simba SC waliingia moja kwa moja na kwenda kuzunguka kibendera kisha kurejea chumbani kwao

Amepatia; Lakini matokeo tu, kwa mshindi amechemsha ilikuwa kinyume

Swaga za mashabiki wa Yanga SC

Ujumbe wa Ngassa

Ngassa mwingine alikuwa jukwaani

Yanga SC ina mashabiki hadi Wazungu

Shabiki

Rais wa TFF, Leodegar Tenga akimvalisha Medali Nahodha wa Yanga SC, Nadir Haroub 'Cannavaro'

Swaga za mashabiki wa Yanga SC

Kigogo wa Yanga SC, Seif Ahmad 'Magari' akiwa amebeba Kombe na kushoto na Simon Msuva

Ameopoa; Mwenyekiti wa kamati ya Ushindi Yanga SC, Abdallah Bin Kleb akiwa na shabiki wa Yanga aliyeigiza kama Mlezi wa Simba SC, Mama Rahma Al Kharoos maarufu kama Malkia wa Nyuki 

Wakili Said El Maamry akisalimiana na Ngassa

Refa Mrtin Saanya akiangalia saa yake mara baada ya kuinuka kutoka kutibiwa kabla ya kumaliza mpira

Refa Saanya hoi chini

Jopo la Madaktari likimuangalia refa Sanya baada ya kumtibu

Alitamani aingine uwanjani kucheza; Nahodha wa zamani wa Simba SC, Suleiman Matola jukwaani

Tenga akimvalisha Medali mtoto wa Haruna Niyonzima kwa niaba ya baba yake

Mzee El Maamry akimvalisha Medali Frank Domayo

Wauwaji; Tenga akimvalisha Medali, Hamisi Kiiza huku Didier Kavumbangu naye akijiandaa kuvalishwa

Kuna wakati Juma Kaseja aliumia na kutishia amani uwanjani, baada ya kuokoa shuti la mpira wa adhabu wa Nizar Khalfan. Kaseja alijaribu kudaka, lakini mpira ukampita na kugonga mwamba kisha ukarudi kumgonga kisogoni, ndipo akaanguka na kuonekana kama aliyepoteza fahamu. 

Didier Kavumbangu akitafuta mbinu za kumtoka Shomary Kapombe 

Didier Kavumbangu kulia na Haruna Niyonzima kushoto wakimdhibiti Mrisho Ngassa

Yanga na Kombe lao...raha iliyoje

No comments:

Post a Comment