Saturday, August 10, 2013

SHEIKH PONDA AJERUHIWA MORO KWA RISASI

Muda wa kama dakika 20 zilizopita mjini Morogoro, Sheikh Ponda amepigwa risasi.

Dhahama hiyo imempata baada ya kushuka kwenye taxi ambako kulikuwa leo akiendesha mhadhala baada ya mhadhala huo kukawa kama kuna maandamano kueleke barabarani, gafla polisi walitokea na kuanzanza kutawanya wakati huo yeye alikuwa hayupo.

Ndipo muda mdogo akawasili akashuka na akapigwa risasi.




---------------
UPDATE 1:
---------------

Haijulikani hali yake. RPC, Faustine Shilogile, anasema hali ni shwari ila Ponda hajui hali yake Maana polisi walizuia gari la Ponda wamkamate, lakini wananchi wakaanza kushambulia polisi ndipo wakarusha risasi hewani kutawanya watu, lakini wananchi wakamtorosha. Anasema taarifa ni nyingi za uongo, hakuna watu polisi wala hospitali waliozingira na anaomba anayejua alipo atoe taarifa.

============================== ====
UPDATE 2 (Media nyingine za Tanzania):
============================== ====
Quote By Millionea View Post
East Africa Radio

HABARI: Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limekanusha kumpiga risasi Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislam Sheikh Ponda Issa Ponda.

Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro ACP Faustine Shilogile amesema polisi walikwenda kumkamata lakini kwa kusaidiwa na wafuasi wake aliwatoroka na hawajui alipo. Jeshi hilo bado linamsaka na halina taarifa kama yupo hai au la.

TBC1:
Hii habari ni uvumi tu, hakuna kilichotokea!
=========================
UPDATE 3 (Shuhuda):
=========================
Quote By Zantsan View Post
Kweli nimeshindwa kuamini kilichotoke, sheikh ponda kubigwa risasi. Nilikuwepo pale uwanjani tena nilikuja mapema kabisa na hivyo kushuhudia kila kitu kilichotokea.

Kimsingi sikuona sababu ya Sheikh Ponda kutokewa na tukio baya kiasi kileambacho hakionyeshi ubinaadamu kabisa, utu wetu, uhuru wetu na hata heshima tuliyonayo watanzania kwenye jumuia za kimataifa. Mpaka sasa haieleweki ni nani hasa kampiga risasi Sheikh Ponda, lakini minong'ono ya watu wanasema ni polisi wamehusika. Binafsi pamoja na kufuatilia kwa ukaribu sikuona ilikotokea risasi hata aliyepiga na nilikuwa mbali kidogo na tukio. Ila nilimwona wakati anapandishwa kwenye pikipiki akiwa tayari amekwisha kupigwa risasi. Imewahuzunisha wengi!

Jamaa ameongea kwa muda mfupi sana ni takribani dakika 18, kwani alianza kuongea saa 11:54 na alimaliza kuongea saa 12:12 jioni. Hali ya uwanjani kwakweli ilikuwa shwari sana, hata polisi hawakuonekana jirani walikuwa kwa nyuma kabisa huku wakiwa wamejisheheni kwa zana zote za kazi.

Mara baada ya ponda kukaribia kumaliza kuongea alisema kuwa muda hautoshi isipokuwa ilitangaza kuwa kesho baada ya swala ya adhuhuri atakuwa kwenye msikiti wa mkoa wa morogoro wa Boma road ambapo ataongea kwa kirefu hivyo kuwataka waislamu kesho kuhudhuria Boma road.

Inavyooneka polisi walipanga wamkamate hata kabla ya kuongea katika ule mkutano na ndio maana walitega sehemu kana kwamba walikuwa wakimsubiri aingie wamkate. Lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi Sheikh Ponda iliingia uwanjani kupitia upande wa pili ambapo msafara wake ulikuwa na gari moja tu na taksi mbayambaya kiasi kwamba wala huwezi kudhania. Mara tunashangaa gari imesimaa na Sheikh Ponda na Amiri wa wahadhiri Tanzania Sheikh Kondo Bungo wakashuka,wakapita kwenye kundi la waislam kwa nyuma ghafla kivumo cha shangwe na Takbir kikavuma huku umati wa waislam waliohudhuria hapo ukiitia allahu akbar, allahu akbar nk.

Wakati huu jukwaani alikuwa akiongea Sheikh Said Riko na ndio aliyewapokea kwa kuanzisha takbir ambayo iliitikiwa na waislam allahu akbari,allahu akbar, allahu akbar. Kwa sababu waliingia kwa kuchelewa ilibidi mara moja Sheikh Said Rico ampishe sheikh Kondo Bungo,amir wa wahadhiri Tanzania aongee. Wakati anaendelea kuongea kabla hata hajamaliza umeme ukakatika, likachukuliwa jenerata ambalo lilikuwa jirani likawashwa, na muhadhara ukaendelea kama kawaida. Sheikh Kondo Bungo akamaliza mada yake, akarudi Sheikh Said Riko, akaongea na kuchangisha michango kwa ajili ya kuendeleza harakati kwa muda wa kama dakika tano hivi ndipo akaruhusiwa Sheikh Ponda kupanda jukwaani.

Sheikh Ponda mara baada ya kumaliza kuongea, watu wakaanza kutawanyika, lkn ghafla mwendesha shughuli akatangaza waislam wasitawanyike kwanza kwa kuwa kulikuwa na matangazo.Wakati matangazo yanendelea ambayo sikuweza kuyasikia , ghafla tukaona defenda moja ya polisi inaingia ambayo ilikuwa imejaza polisi walio tayari kwa mapambano. Waislam wakawa wanawashanga kulikoni tena ilhali mkutano ulifanyika na kuisha kwa amani kabisa.

Basi Sheikh Ponda akaingizwa kwenye taxi iliyokuja kumfuata akiambatana na Sheikh Kondo Bonge. Polisi walitaka kumkamata sheikh Ponda lakini waumini wakamkinga kwa kulizingira gari alilopanda sheikh Ponda huku likiondoka taratibu. Huku nyuma gari la polisi likawa linafuata taratibu bila kubiga risasi hewani wala kupiga mabomu ya machozi. Gari ya polisi ilipofika barabara ya lami maeneo ya karibu na jengo la Fire ilionekana kusima kwa muda huko gari iliyombeba sheikh Ponda kukunja kushoto kueleke kwenye msikiti wa Mungu mmoja dini moja. Kabla msafara wa Ponda haujafika kokote gari nne za polisi zilikuja kwa kasi sana na kuanza kupiga mabomu ya machozi kuwatawanya waumini, watu walitawanyika na Sheikh Ponda akashuka na kuelekea kwenye Gereji moja hivi kabla ya kufika idara ya maji ambako ndiko alikopigwa risasi. Kwakweli sijui ilikotoke risasi iliyompiga Ponda, nadhani kamanda wa polisi atalitolea ufafanuzi zaidi. Mimi nimeandika kile nilichoona kwa macho yangu!

Mi nilidhani ingekuwa busara kwa jeshi la polisi kama walimuhitaji sheikh ponda wangemwambia anahitajika polisi na hivyo ajisalimishe.
=========================
UPDATE 4 (Shuhuda #2):
=========================
Quote By Maulid Daniel View Post
Ndugu,

Nipo Morogoro na kwenye Ule muhadhara wa Sheikh Ponda nilikuwepo. Ilipofika saa 12:15 Sheikh ponda akahitimisha na kusema wanakwenda kuswali ktk msikiti unaitwa Mungu Mmoja dini moja maeneo ya kiwanda cha tumbaku mawenzi.

Tukiwa njiani tunakimbilia gari lake ghafra askari wakatuzingira sehemu yenyewe ni maeneo ya garage panaitwa Kwa Muki ndipo Sheikh ponda akashuka kwenye gari na police kuanza kwa kupiga mabomu ya machozi.

Aliyempiga Sheikh Ponda alikuwa ni police na alikuwa kwenye gari la FFU na amevalia sare kabisa
============================== ===========
UPDATE 5 (Vyombo vya Habari vya Nje):
============================== ===========
By Mike Pflanz, Stone Town | The Telegraph (UK) | 6:24PM BST 10 Aug 2013

Sheikh Issa Ponda is understood to have survived the raid and was on the run but injured, police sources told The Daily Telegraph.

He had visited Zanzibar in the weeks running up to the attack on Katie Gee and Kirstie Trup, both from north London, who were on Saturday still in hospital being treated for their injuries.

Ponda earlier this month met with the imprisoned leaders of a Muslim separatist group, Uamsho, who police believe may have inspired the attack on the two women.

Tanzania’s director of public prosecutions, Elieza Feleshi, on Friday ordered that the cleric be arrested after accusing him of inciting violence, for which he was convicted earlier this year and given a 12 month suspended sentence.

“He narrowly escaped from the police in Morogoro, he was shot by our officers, but we are pursuing him,” said Faustine Shilogile, a senior police commander in Morogoro, the town 110 miles west of Tanzania’s commercial capital, Dar es Salaam, where Ponda was shot.


The Telegraph: Radical preacher wanted over Zanzibar acid attack shot in police raid - Telegraph

Other sources:

1. The Mirror: Zanzibar acid attack: Hate cleric Sheikh Issa Ponda Issa shot and captured by police in Tanzania - Mirror Online

2. Top News Today: Top News Today | Zanzibar acid attack: Hate cleric Sheikh Issa Ponda Issa shot and captured by police in Tanzania | Uk | mirror.co.uk

3. News UK: Zanzibar acid attack: Hate cleric Sheikh Issa Ponda Issa shot and captured by police in Tanzania

No comments:

Post a Comment