JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro
linamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 15 mwanafunzi wa kidato cha
pili katika shule ya sekondari Kelamfua iliyopo wilayani Rombo baada ya
kukutwa akimwingilia ndama wa ng’ombe.
Akithibitisha, Kamanda wa Polisi wa mkoa
wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema tukio hilo lilitokea Agosti 3 mwaka
huu saa 5:10 usiku nyumbani kwao Kelamfua.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana huyo ndiyo aliyemfumania kwa kuwa alikuwa akimfuatilia kwa muda mrefu na ndipo alipomkamata.
Alisema kuwa kabla ya tukio hilo kijana
huyo aliwahi kukutwa akifanya mapenzi na kuku na kuanzia hapo mzazi wake
huyo akaanza kumfuatilia na hivyo kumkamata akifanya mapenzi na ng’ombe
ambaye ni ndama.
Kamanda alisema kuwa baada ya kukamatwa
kijana huyo alifikishwa kituo cha polisi na kuhojiwa ambapo alikiri
kufanya kitendo hicho na kueleza kuwa amekuwa akitafuta wasichana bila
mafanikio.
Aidha aliongeza kuwa kila msichana
anayemtakia neno la mapenzi amekuwa akitaka fedha nyingi wakati yeye ni
mwanafunzi hana uwezo wa kupata fedha.
Boaz alisema kuwa baba wa kijana huyo
alishapata taarifa siku za nyuma kuhusiana na tabia ya kijana wake huyo
na ndipo akaanza kumfuatilia na kwa sasa anashikiliwa na polisi
uchunguzi zaidi ukiendelea
No comments:
Post a Comment