LICHA ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watu wengi kuogopa kufanya maovu, jimama anayekwenda kwa jina la Joyce Benson (34), amefumwa akifanya ngono katika makaburi ya Malapa, Buguruni jijini Dar.
Jimama likiojiwa na Askali polisi
Joyce amekamatwa usiku wa kuamkia Alhamisi iliyopita saa nane katika
maeneo hayo akifanya biashara haramu ya kuuza mwili wake katika makaburi
hayo kwa njia ya kujipatia fedha.Joyce mwenye umbile la miraba minne alipatwa na fedheha kubwa baada ya majirani zake kusikia habari hizo na kuanza kumlaani.
Mbali na Joyce pia siku hiyo machangudoa wengine 14, waliokuwa wakifanyia vitendo vya ukahaba kwenye makaburi hayo walikamatwa.
Wakiwa mahakamani hapo, mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi aliwasomea tuhuma za kufanya ukahaba na kumfanya hakimu wa mahakama hiyo, Timoth Lyon kupigwa na butwaa.
Licha ya dhamana kuwa wazi, jimama huyo alijikuta akipandishwa kwenye karandinga na kupelekwa Gereza la Segerea baada ya kukosa mdhamini huku baadhi wakichomolewa na wadhamini wao.
No comments:
Post a Comment