Na: Meshack Maganga-Iringa.
Kwa
muda mrefu nimekuwa nikitoa hamasa kwa vijana wenzangu wa kike na kiume
na watu wa kada mbalimbali, wito wangu umekuwa nikuwataka vijana
wenzangu kuanza utamaduni wa kuwekeza kwa muda mrefu na kujifunza
ujasiriamali. Ninaandika kutoa ushuhuda wa niliyoyafanya kwa muda wa
miaka miwili iliyopita,na pia ninaandika makala hii kujibu baadhi ya
maswali ambayo baadhi ya rafiki zangu wamekuwa wakiniuliza. Nilianza
kujishighulisha na ujasiriamali nilipokuwa chuo kikuu mwaka wa pili, kwa
kuuza vocha na kazi ya 'steshenari' chumbani kwangu, na uuzaji wa
laptop, sikuendelea nazo sana kwa sababu ya kubanwa na masomo ya chuo.
Nilipomaliza chuo 2010, nilianza kilimo cha mboga na kufuga kuku hapa
Iringa mjini,baada ya hapo kaka yangu alianza kunihimiza kuhusu kilimo
cha miti ambacho yeye mwenyewe anafanya. Na baadae nikakutana na rafiki
yangu Albert Sanga ambae anafanya pia kilimo cha miti kwa sana.Katika
insha yangu ya mwaka 2012, niiliyoipa kichwa cha.... SOMA ZAIDI HAPA CHINI...
'KWENYE UJASIRIAMALI NG'OMBE WA MASIKINI HUZAA' nilisema kwamba, Maisha
ni magumu sawa,mifumo ya nchi ni mibovu sawa,uchumi wa nchi unaporomoka
sawa lakini haiwezi kuwa na madhara katika roho ya binadamu aliyeamua
maisha yake. Mambo ni mengi yanayoweza kuturudisha nyuma lakini ukirudi
nyuma ni maamuzi yako wewe na si mambo yanayokuzunguka. Na kwenye Makala
yangu nyingine ya mwaka huhuo 2012 Yenye kichwa cha MAISHA BILA MAARIFA
NI SAWA NA GARI LISILO NA MAFUTA. Nilisema kwamba, binadamu ana mambo
matatu muhimu ambayo anaweza kuyaendesha au yakamwendesha kichwani
kwake, moja ni fikra zake au mtazamo(thoughts you think),mbili ni
taswira anazozijenga kichwani kwake(image you visualize) na tatu ni
vitendo vyake (the actions you take).
Niliamini
kwamba,maisha ya baadae hayaandaliwi baadae, maisha ya baadae
yanaandaliwa sasa. Tangu 2011 nilinunua shamba la ekari 10 na kuzipanda
miti hela ambayo niliipata baada ya kuuza matango niliyolima kijijini
Kalenga,nikaongeza bidii zaidi ya kulima matango na kununua mashamba,leo
nina ekari nyingi.
Yupo
mjasiriamali mmoja alipata kusema kwamba,mtanzania zinduka, usiseme
hakuna pesa, pesa zipo nyingi sana, fursa za kumwaga,na usisubiri
serikali ikufanyie kila utakacho kwani ulikuja duniani ili ubebwe na
serikali? Kwa sasa tupo watanzania milioni 44 wote tukisubiri kubebwa
tutakuwa taifa la aina gani hili?
Albert
sanga, mjasirimali na mwekezaji alipata kuandika haya kuhusu
mimi:-"UNASUBIRI UPATE MTAJI? OPSIII! UNAWEZA KUFA MASIKINI! Nina rafiki
yangu mpambanaji kweli kweli na msomi wa chuo kikuu wa mambo ya
maendeleo na elimu; na mtaalamu wa IT, anaitwa Meshack Maganga. Wakati
fulani huko nyuma alinifuata na kuniambia, "Sanga nimeamua kuanza
kui-invest katika mashamba ya miti; mtaji wa kuanzia nina tsh elfu
ishirini na tano, (25,000?/=). Nikamwambia "Kupata ekari moja si chini
ya laki sita na wewe una tsh 25,000/= utawezaje?" Akanijibu "Nitaweza!",
Sikumwelewa! Kumbe alikuwa anaona mbali! Alichofanya alichukua hiyo
25,000/= akaenda nayo eneo moja linaitwa Kalenga (km 20 kutoka Iringa
mjini) huko akalima matango. Angalia mchanganuo: Shamba nusu eka akakodi
kwa tsh 10,000/=, mbegu za matango akanunua tsh. 7,000/=. Kwenye kulima
akalima kwa mikono yake akisaidiana na kibarua mmoja. Fedha iliyobaki
8,000/= akalipa kibarua na kununulia dawa ya kuua wadudu. Alipokuja
kuvuna akapata tsh 800,000/=(laki nane). Alipokuja na fedha hii tukaenda
kutafuta shamba la miti akaanza na ekari moja huku pesa nyingine
akairudisha shambani. Hivi leo Bw. Maganga ana ekari zisizopungua
hamsini za mashamba ya miti na anaendelea na kilimo cha umwagiliaji.
Lakini HAPO amefika kwa kutumia tsh 25,000/= tu. Tunaposema hauhitaji
mamilioni kujiajiri tunatamani ujifunze kutoka kwa waliofanikiwa kama
Bw. Maganga. Unaweza kumwandikia" Akaendelea kwa kusema:-
Kuhusu kilimo cha miti ninacho kifanya mimi na nimepania kwelikweli ndani ya nchi yangu niipendayo Tanzania ni kwamba, kimepata umaarufu wa ghafla miaka ya hivi karibuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ongezeko la mahitaji ya mazao ya miti na changamoto ya mazingira. Katika Tanzania mkoa wa Iringa ni moja ya mikoa maarufu inayoongoza kwa misitu mikubwa ya kupandwa. Miti inatumika kwa mbao, nguzo za umeme, nguzo za kujengea pamoja na utengenezeaji wa karatasi.
Ukiacha
mahitaji haya tuliyoyazoea; hivi sasa kumeibuka fursa nyingine mpya
ambapo mashirika ya kimazingira kutoka Magharibi yananunua hewa ukaa.
Kwa maana hiyo unaweza kupanda shamba la miti halafu ukawa unakusanya
dola kwa kuuza hewa ukaa wakati ukisubiri miti ikomae uvune mbao, nguzo
ama miti ghafi ya kutengenezea karatasi.(Hii ni sawa na kutegeneza hela
ukiwa umelala) Mbali na kuuza hewa ukaa, vile vile unaweza kufuga nyuki
na kuendelea kuvuna asali wakati unasubiri kukusanya mamilioni kwa kuuza
miti ya nguzo, karatasi ama mbao
Kilimo
hiki cha miti ni uwekezaji wa muda wa kati na mrefu (middle& long
term investments). Kiutamaduni watanzania wengi huwa hawavutiwi na
uwekezaji wa muda mrefu. Hata hivyo kama una mpango wa kuwa na
"financial freedom" usikwepe kufikiria uwekezaji wa muda mrefu.
Waingereza husema "Information is power". Wengi hawajachangamkia fursa
hii kwa kukosa taarifa tu. Kazi yangu leo ni kukupa taarifa hizi za
utajirisho.
Miti
ya mbao inatumia wastani wa miaka sita hadi 8 au saba, tangu kupandwa
hadi kuvunwa kwake. Hii ina maana inapofikisha umri wa miaka sita huwa
tayari kwa kuanza kuvunwa kwa mbao ndogo. Ekari moja ya shamba inachukua
wastani wa miti mia sita (600). Wastani wa chini wa mti mmoja kwa sasa
uliokomaa ni shilingi elfu ishirini (30,000 hadi 60,000,inategemea na
ukubwa wa mti). Ina maana katika ekari moja ukiwa na miti iliyokomaa
unakusanya jumla ya shilingi milioni kumi na mbili (18,000,000).
Fedha
hiyo (kadirio la chini kabisa) utaipata ikiwa unaamua kuuza kwa bei ya
jumla miti ikiwa shambani. Lakini kama ukiamua kupasua mbao wewe
mwenyewe unaweza kuvuna mbao hadi za milioni ishirini na tano
(32,000,000) kwa ekari moja. Hadi sasa uhitaji(demand) wa mbao katika
soko ni mkubwa kuliko ugavi (supply) hivyo kwa miaka 10 ijayo
hatutarajii kushuka kwa soko la mbao, nguzo ama malighafi za karatasi.
Gharama
ya kununua shamba tupu ni kati ya shilingi laki moja na 20 elfu
(120,000) na laki moja,kutegemea na maeneo husika unayotaka ama kupata.
Gharama za kuandaa shamba, kununua miche na kupanda ni kati ya shilingi
laki moja na nusu,na laki moja. Hii ina maana unaweza kumiliki ekari
moja ya msitu wa miti kwa hadi shilingi laki sita tu! Kutegemea na umri
wa miti unayotaka.
Mtu
unaweza kuona kuwa pengine kununua shamba tupu na kuanza kuhangaika na
upandaji miti itakuwa ni mlolongo mkubwa; kukusaidia katika hilo
nimekuwa na utaratibu wa kumilikisha mashamba yenye miti (kuuza) kwa bei
nafuu sana.
Kilimo
cha miti ni rahisi sana kwa sababu ukishapanda hakihitaji uangalizi
mkubwa sana na wala hauhitajiki uwe karibu na shamba/mradi muda wote.
Kuna kazi chache ambazo zinahitajika ukishapanda shamba lako. Mvua
inyeshe ama isinyeshe mti wa mbao, nguzo ama karatasi ukishachipua huwa
haufi kwani huendelea kutumia unyevu wa ardhini.
Kazi
namba moja unapokuwa umeshakamilisha upandaji wa miti kwenye shamba; ni
kutengeneza njia za kuzuia moto walau mara moja kwa mwaka, kazi ya pili
ni kufyekea miti inapokua walau kwa mwaka mara moja (prooning). Gharama
zote hizo yaani kutengeneza njia za moto, kufyekea na kulinda moto
haizidi laki mbili kwa mwaka mzima.
Kwa
maana hii gharama za kuhudumia shamba la miti ekari moja kutoka
kupandwa hadi kuvunwa ni wastani wa shilingi milioni moja tu. Gharama
hizi ninazopiga ni ikiwa utaamua kununua shamba leo na kama ungekuwa
tayari una shamba ambalo unalihudumia leo.
Hata
hivyo nadhani wote tunafahamu kuwa ardhi ni rasilimali inayopanda
thamani kila siku. Vile vile tunatambua kuwa suala la mazingira ni tete
kwa sasa na katika karne zijazo kama wataalamu wanavyotuthibitishia. Hii
ina maana kuwa ukiwa na shamba la miti leo; thamani ya ardhi hiyo
inazidi kupanda kila siku na miti uliyopanda inazidi kupanda thamani
kila kukicha.
Jambo
la uhakika ni kuwa hata kama bei ya miti, mbao, nguzo itayumba hutaweza
kupoteza mtaji uliotumia na wala hutakosa kuzalisha faida kwa shamba
utakalokuwa umemiliki, iwe ni eka moja, kumi, mia ama elfu moja. Mbali
na hivyo unaweza ukaona, ahaa, miaka sita hadi kumi ni mingi mno; bado
una nafasiya kupata faida hata ndani ya mwaka mmoja, miwili n.k.
Ukishapanda
shamba la miti ekari moja kisha baada ya mwaka mmoja ukaamua uuze
utauza si chini ya milioni mbili hadi nne. Kukusanya milioni nne kwa
mtaji wa laki sita, pasipo kutumia muda mwingi ama usumbufu wa
kusimamia; hakika ni faida nono.
Huenda
hadi kufika hapa unaweza ukawa umeshavutiwa na biashara hii. Wengi wenu
mnaweza kujiuliza maswali mkubwa mawili; "Ninatamani nifanye mradi huu
lakini Iringa sikufahamu na hata kama nakufahamu nitaanzia wapi kupata
hayo maeneo?" Pili: Niko mbali na sina muda wa kushinda Iringa, Je, ni
nani atanisaidia kupanda, kusimamia na kuendesha hayo mashamba?
Ili
kutimiza ndoto yangu hiyo nimeweka utaratibu ufuatao utakaohakikisha
kila mwenye ndoto, kiu na hamasiko la kuwekeza kwenye kilimo cha miti
anafanikiwa. Jisikie huru wakati wowote kuwasiliana nami kwa ufafanuzi
na msaada wa fursa hii. Natamani watanzania tuache kulalamika kuhusu
wageni kuvamia ardhi yetu, badala yake tuchangamke kumiliki na kufanya
uzalishaji katika ardhi yetu. Inawezekana!
Kwa
kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 sheria namba 5 utapata documents
za umiliki; kwa kuzingatia taratibu na tamaduni zote za wenyeji
zinazohusiana na umilikaji ardhi nitahakikisha nakusaidia ili ndoto yako
itimie.
Yupo
Baba yangu anaishi Mafinga ambae siku za karibuni amepewa Tuzo ya Rais
kwa kuwa mpandaji namba moja wa miti na utunzaji wa mazingira,ameahidi
kutoa msaada kwa Mtanzania wa ndani na nje ya Tanzania kumsadia kupata
eneo la kupanda miti na kauli yake siku zote ni "USIKUBALI KUWA MNYONGE WA KIUCHUMI NDANI YA TANZANIA.NA UWEZO WA KUJUA KAMA TUTAKUFA MASKINI TUNAO
meshackmaganga@gmail.com. 0767 48 66 36
meshackmaganga@gmail.com. 0767 48 66 36
No comments:
Post a Comment