Hata hivyo alisema baada ya kutoka
nje na kuelekea eneo hilo ambalo sauti ilisikika alishuhudia kijana
huyo akiendelea kumbaka mtoto wake jambo lilopelekea kupiga kelele
kuomba msaada kwa wananchi ili kusaidia kumkamata mtuhumiwa huyo wa
ubakaji.
Mwanamke huyo alisema kuwa
jitihada za wananchi wa eneo hilo la Mwangata kumkamata mtuhumiwa
ziliweza kufanikiwa pamoja na mtuhumiwa huyo kutaka kujaribu kukimbia
eneo hilo.
Mmoja kati ya wananchi
walioshiriki kumkamata kijana huyo mbakaji aliyejitambulisha kwa jina
la Samweli kalinga alisema kuwa kijana huyo amekuwa na tabia ya
kuwabaka watoto katika eneo hilo la Mwangata na mara nyingi watoto
wamekuwa wakibakwa ila walikuwa hawajui ni nani anayeendesha vitendo
hivyo vya ubakaji .
Mtuhumiwa huyo amefikishwa katika kituo kikuu cha polisi mjini Iringa huku akiwa hoi kwa kichapo na kupelekea kuvuja damu kupita kiasi kichwani kutokana na kichapo alichokipata kutoka kwa wananchi.
Toka kwa; Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::
No comments:
Post a Comment