Thursday, May 9, 2013

VIONGOZI WA SAFIA WAPANDISWA KWA PILATO

safia a6559
Askari  polisi akiwaongoza viongozi  wa Chama cha wavunaji wenye Viwanda vya Mbao katika msitu wa Taifa wa Saohill Mufindi (SAFIA),mwenyekit, Wiliam Nyalusi (64), katibu, Osca Kaduma (42) na mjumbe Donald Ndalo(45) wakipelekwa mahabusu ya makama ya makimu mkazi mkoa wa Iringa.

VIONGOZI wa juu wa Chama cha wavunaji wenye Viwanda vya Mbao katika msitu wa Taifa wa Saohill Mufindi (SAFIA),mkoani Iringa akiwemo katibu na mwenyekiti, Wiliam Nyalusi (64) jana wafikishwa mahakamani kwa makosa matatu likiwemo la kughushi nyaraka .

Akisoma mashtaka hayo mbele hakimu mkazi ,mwandamizi mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Iringa Juma Hasan , wakili wa serikali Adolph Maganda aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Wiliam Nyalusi wengine ni Osca Kaduma (42) na Donald Ndalo(45).
Wakili Maganda alisema kuwa washitakiwa hao watatu kwa pamoja wamefikishwa mahakamani hapo kwa makosa matatu yanayowakabili likiwemo kosa la kwanza la kula njama kinyume na kifungu 484 cha sheria ya kanunia ya adhabu sura ya 16 kanuni iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kosa la pili ni kughushi kinyume na kifungu namba 333/335 kifungu kidogo D (1) na kifungu 337 wakati kosa la tatu ni kughushi nyaraka .
Wakili Maganda alisema kuwa kwa pamoja washtakiwa hao mwezi Februari mwaka 2011 na mwezi April 2013 wakiwa katika eneo la Sao Hill Mufindi walikula njama na kutenda kosa na April mosi mwaka 2011 kwa pamoja wanadaiwa kughushi nyaraka ambazo ni vocha kwa kuweka sahihi ya mtu anayetambulika kwa jina la Kalinga jambo ambalo ni kosa .
Pia viongozi hao Februari 10 mwaka 2011 wakiwa huko huko katika eneo la Sao Hill walighushi nyaraka kwa kusaini vocha na kuonyesha kuwa nyaraka hizo zimesainiwa na Awad Shepha jambo ambalo ni kosa pia na kuwa umepelezi bado haujakamilika.
Washitakiwa wote watatu walikana mashitaka yote dhidi yao na mahakama hiyo kudai kuwa dhamana kwa washitakiwa hao ipo wazi kwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili wakazi wa mkoa wa Iringa akiwemo mmoja mwenye dhamana isoyohamishika yenye thamani ya kuanzia kiasi cha Tsh milioni 10. Kesi itatajwa Mei22, 2013. Chanzo: Francis Godwin

No comments:

Post a Comment