Wakati
bado kuna maswali mengi kuhusu magaidi waliohusika na shambulio la
Westgate kama kweli waliuawa kama isemavyo taarifa ya serikali ya Kenya,
mtandao wa Mirror umetoa taarifa kuhusu tetesi za uwezekano wa magaidi
hao kutorokea njia ya maji taka kutoka katika jengo hilo.
Ripota wa Sunday Mirror Russell Myers akiwa ndani ya handaki lenye njia ya maji taka kutokea jengo la Westgate
Mtandao
huo umedai kuwa baadhi ya magaidi walitoroka kupitia njia ya maji taka
iliyoko chini ya jengo la Westgate inayoenda kutokea katika mto Nairobi.
Kwa
mujibu wa habari hiyo njia hiyo inaanzia eneo la maegesho ya magari
katika jengo la Westgate na inaenda moja kwa moja kutokea katikati ya
jiji la Nairobi. Magaidi hao wanahofiwa kutumia njia hiyo ya maji taka
kutoroka na kuwaacha wengine wakiendelea kushambulia.
Hapa ndipo inapotokea njia hiyo ya maji taka kutoka Westgate hadi katikati ya jiji la Nairobi
Taarifa
hiyo inaendelea kudai kuwa wana usalama wanadai kuwa magaidi wa
Al-shabaab walisafiri umbali wa nusu maili kwa magoti katika njia hiyo
ya chini ya ardhi katika njia ya maji taka.
Chanzo kimoja kilisema “They
escaped like sewer rats. The terrorists would have been able to pass
through the underground tunnels at a rapid pace and surface almost
unnoticed”.
Taarifa
hiyo inaendelea kusema kuwa wachunguzi wa Kenya hawakuigundua njia hiyo
ya kutorokea mpaka masaa 72 kupita baada ya shambulio kutokea.
Unaweza kuisoma taarifa hiyo kwa undani hapa
Source: Mirror
No comments:
Post a Comment