sehemu ya meza kuu.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri akizungumza na wakazi wa mji
wa Iringa na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye semina ya kamata fursa
twenzetu,ASAS amejitolea kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya
kusaidia vikundi vitakavyoamua kutumia fursa ya kulima vitunguu na
kuendelea kuwa wajasiliamali katika fursa mbalimbali.
Mfanyabiashara
mkubwa wa mjini Iringa,Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim
Abri akionesha baadhi ya fursa zilizopo mkoani Iringa kwa kuonesha
kitunguu cheupe kama moja ya bidhaa za thamani zinazopatikana mkoani
humo,ASAS ameeleza kuwa vitunguu hivyo vinauzwa kwa kilo kwenye
SuperMarket nyingi,anasema kuwa vitunguu hivyo vinadaiwa kutoka nje ya
nchi,lakini vitunguu hivi inawezekana kuvipanda hapa mkoani Iringa na
vijana wakanufaika kupitia mradi wa vitunguu hivyo.
Mdau
mkubwa wa michezo nchini Fredrick Mwakalebela naye alipata wasaa wa
kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja
kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakaoweza kutumia fursa ya
rasilimali zilizopo mkoani hapo.
Msanii
wa kughani mashairi Mrisho Mpoto, akizungumza na wakazi wa Iringa
waliojitokeza kusikiliza mafunzo ya namna ya kujikwamua kimaisha kwa
kutumia fursa kwa rasilimali zilizopo mjini Iringa.
Baadhi
ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi
wa Chuo cha Mtakatifu Dominic mjini Iringa,ambapo watu mbalimbali
wamepata fursa ya kujua namna ya kutumia sasilimali zilizopo mkoni humo
kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.
Mwakilishi kutoka NSSF Makao
Makuu Salim Khalfan, akizungumzia Fursa kwa upande wa NSSF wanavyoweza kuitumia
wakazi wa Iringa katika kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.
Mkurugenzi
wa vipindi na
uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya
Kamata fursa twenzetu mepema leo mchana ndani ya mkoa wa Iringa.
Baadhi ya Wadau mbalimbali wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwey´nye Semina ya kamata fursa kwa vijana twenzetu.
Wanafuatilia.
No comments:
Post a Comment