Staa
wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo,Rehema Chalamilla 'Ray C', akiingiza
sauti ndani ya Studio za THT, chini ya maprodyuza Emma The Boy na Tudy
Thomas,ambao wamepania kumrejesha katika game kwa kishindo msanii huyo,
ambaye alipotea kwenye ulimwengu wa Burudani baada ya kutopea katika
utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa sasa ameachana nayo na kumrudia
mwenyezi Mungu sambamba na kuendelea kutumia dozi ya kuondoa sumu ya
madawa hayo.
Ray C akiingiza sauti tayari kwa maandalizi ya ujio mpya kwenye game la Bongo Fleva.
Prodyuza
Tudy Thomas (kulia), akijadiliana jambo lililotokana na majadiliano ya
kuboresha ngoma mpya ya Ray C, pichani kati ni Emma The Boy akipiga
mzigo tayari kwa kumkamilishia Ray C ngoma yake mpya ambayo anatarajia
kuiachia hivi karibuni.
Ray C, akijaribu kutoa akapela kwa Maprodyuza hao, wakati wakiendelea kuiboresha ngoma yake mpya.
Ray C, Emma The Boy &Tudy Thomas ndani ya Studio
Ray C, akiwa katika pozi ndani ya studio hiyo.
No comments:
Post a Comment