Wanaume
wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata suluhu
ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda Wamesaini mkataba
wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao. Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angelifunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini walipogunduana , ilikuwa ni
ugomvi wa mara kwa mara lakini mwanamke huyo alipoambiwa amchague mnmoja
wao, alishindwa. Akasema anawapenda wote wawili.
Na baada ya hapo watatu hao
waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu wanaume hao wawili kuishi
na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila mmoja wao atakuwa na wakati
wake wa 'kwenda kumjulia hali.'
Vile vile mkataba huo unawashurutisha
kugawana majukumu yote ya nyumbani ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na
kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa na haki sawa.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za
kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na wanaume wawili na mkataba huo
sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria, huku sheria mpya ya ndoa
ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
No comments:
Post a Comment