Mrembo Yvonne aliyempasua kwa chupa Aunt Ezekiel usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas.
Pichani juu ni mrembo aliyempasua
mwigizaji wa sinema za Bongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ ajulikanaye
kwa jina la Yvonne. Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Jumatatu, nje
ya Ukumbi wa Billicanas, ambapo Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya
bia na kumpasua mkono wa kushoto. Vurugu kubwa ilizuka baada ya tukio
hilo na Aunt alikimbizwa hospitali ya Aga Khan huku Yvonne akapelekwa
msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.
No comments:
Post a Comment