Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam
leo Kamishina wa Tume ya Kuratibu na Kuthibiti Dawa za Kulevya nchini,
Christopher Shekiondo alisema kwamba inaonesha Watanzania wengi wamekamatwa
na dawa za kulevya nchini Brazil ambao idadi yao inafikia 109, ambapo
wengi wao wameshahukumiwa.
Alisema watu hao wamekamtwa nchini
humo, wakiwa na dawa aina ya cocain kwa ajili ya kusafirisha nchi
nyingine, huku baadhi yao wamehukumiwa kunyongwa pamoja na kifungo cha
maisha, ingawa idadi kamili ya watu hao bado haijafika rasmi.
"Tumepokea
taarifa jumla ya Watanzania 109 wamekamtwa nchini Brazil, ingawa bado
tunasubiri kujua ni wangapi waliohukumiwa kifo, pamoja na kifungo cha
maisha," alisema Shekiondo.
Aliongezea kuwa baadhi ya nchi
nyingine, ambazo Watanzania wanakamatwa na dawa hizo za kulevya wakiwa
wanasafirisha ni China vijana 34, Kenya 30, Pakistani 16, Falme za
Kiarabu ikiwemo Dubai 14, pamoja na nchi nyingine kama Japan,
Argentina, Msumbiji, Afrika Kusini, Ureno, pamoja na Uingereza.
Akizungumzia
hukumu ambazo zimeshatolewa baadhi ya nchi walizokamatwa Watanzania
hao,, Kamishina huyo alisema Brazil ambayo ndiyo Watanzania wengi
wamekamatwa idadi kamili, bado hawajapata ingawa Kenya tayari wapo
waliohukumiwa kifungo cha maisha, huku wengine wakiwa wamehukumiwa
kifungo cha miaka 20 hadi 40, nchi China wapo waliohukumiwa kifo na
kifungo cha maisha.
Shekiondo alisema Tanzania kwa sasa inajulikana kama ni njia ya kusafirisha dawa hizo.
Alisema
kuna baadhi ya watu wanatumia maji kusafirisha dawa hizo, yaani meli,
jahazi pamoja na mitumbwi, hivyo wana mikakati ya kutoa elimu kwa jamii
kuhusu udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment