Thursday, July 25, 2013

SIKU YA MASHUJAA IRINGA

kaimu  mkuu  wa mkoa  wa Iringa Gerald Guninita  ambae ni mkuu wa  wilaya ya  kilolo  akiweka ngao katika mnala  wa mashujaa wa  jimbo la Iringa  waliopoteza maisha katika  vita kati  ya mwaka 1939 -1945  ,kumbukumbu  zilizofanyika leo katika  bustani ya Manispaa ya  Iringa
 Askari mstaafu  SGT Augustino Sambangi ambae ni mwenyekiti  wa askari  wastaafu mkoa  wa  Iringa akitoa heshima  zake katika  mnala  huo leo
  Askari mstaafu  SGT Augustino Sambangi ambae ni mwenyekiti  wa askari  wastaafu mkoa  wa  Iringa akiweka  upinde  katika  mnala  huo
 Askari  na  mgeni rasmi wakitoa heshima zao katika mnala  wa  kumbukumbu ya  mashujaa leo


 Mkuu  wa mgambo  mkoa  wa Iringa COl Sv Shayo  akiweka shime  katika mnala  huo
 Mwakilishi  wa  wananchi  wa mkoa  wa Iringa mzee  Said Mdota  akitoka katika  mnala  huo baada ya  kuweka shoka  la  kumbukumbu










 Wafanyakazi  wa Hospital ya  Rufaa ya  mkoa  wa Iringa  wakiwa  wamepanda  juu ya uzio  kushuhudia kabla ya  kutimua mbio kutokana na milio ya  risasi
 Askari  wa  jeshi la  kujenga  Taifa  (JWTZ)  wakipiga  risasi  hewani kutoa  heshima kwa mashujaa hao


 Heshima kwa mashujaa  waliopoteza maisha  katika vita 
KUMBUKUMBU ya  siku ya mashujaa iliyofanyika   katika  bustani ya Manispaa ya  Iringa kwa  mkoa wa Iringa  imezua hali ya  taharuki  kwa  wananchi  wa mji wa Iringa wakiwemo  wagonjwa  katika  Hospital ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa kutokana na risasi zilizokuwa  zikipigwa na askari  wa jeshi la kujenga  Taifa (KJT) .
Na Mzee wa Matukio.

No comments:

Post a Comment