Monday, July 15, 2013

BUS LA NAJMA LAPATA AJARI


clip_image001
Basi la Kampuni ya Najma yenye makao makuu yake Nachingwea - Lindi, limepata ajali maeneo ya daraja la Mkapa leo mchana. Habari toka kwa mmoja wa wasafiri aliyekuwemo kwenye basi hilo ameiambia ChingaOne blog kuwa basi hilo lenye Namba T599 CBL (Yutong)  lililokuwa linatoka wilayani Nachingwea kwenda Dar es salaam liligonga pikipiki  iliyobeba watu wawili ambao walifariki dunia baada ya ajali hiyo. 
Inasemekana chanzo cha ajali hiyo ni moshi mzito uliotanda eneo la ajali ambao ulisababishwa na moto uliokuwa unawaka pembeni ya barabara hiyo, basi hilo limeumia sana sehemu za mbele ila hadi sasa hakuna taarifa za kuwepo kwa majeruhi yoyote zaidi ya vifo vya watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki.

No comments:

Post a Comment