Thursday, July 11, 2013

AHUKUMIWA MIAKA 5 JELA KWA KUTUPA MTOTO CHOONI

Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari  kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.…
Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari  kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.
Pichani juu ni taswira za wananchi wa eneo la Manga A jijini Mbeya wakati wakijaribu kuokoa maisha ya kichanga  kilichotupwa chooni na Rukia Haruna Juni 14 mwaka huu.
Picha iliyozibwa ni ya kichanga kilichotupwa baada ya kutolewa chooni.
Mwanamke Rukia Haruna (31), mkazi wa Manga A Jijini Mbeya, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa alilazimika kutupa kichanga hicho katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles Mulisa, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula, amemhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kosa hilo ambalo ni kinyume cha kifungu  218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka 2002.
HABARI NA MBEYA YETU BLOG

No comments:

Post a Comment