-Kwa sasa mwili wa marehemu upo katika Viwanja vya Leaders na umefika mahali hapo saa mbili kamili asubuhi
-Zoezi la kuaga mwili wa marehemu bado halijaanza ila litaanza muda wowote
-Watu wanazidi kumiminika katika Viwanja vya Leaders
-Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo ,Dk.Fenella Mukangara
naye anatarajiwa kuwa miongoni mwa watu watakaofika eneo hilo kuaga
mwili wa Mangweha
-Baada ya shughuli za kuaga, mwili wa marehemu
utapelekwa mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika nyumbani
kwao Kihonda hapo kesho
No comments:
Post a Comment