Tuesday, June 18, 2013

Binti Mtanzania aliyekamatwa Misri akituhumiwa kusafirisha dawa za kulevya

Kwa mujibu wa tovuti ya SalmaMsangi.com, yupo binti kwa jina Fatma almaarufu huko Ilala, Dar es Salaam kwa jina la Brown Berry ambaye inasemekana amekamatwa nchini Misri kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya.

Link ya video (imepachikwa hapo chini) iliyowekwa na mmoja wa watoa maoni kwenye mtandao wa Instagram baada ya SalmaMsangi kuweka maelezo na picha ya mtuhumiwa, inaonesha mfuko wa plastiki ukiondolewa chini ya sanduku dogo ukiwa na kitu kama “unga” ndani yake.

Habari kutoka Jjestina-George.com zinasema William Malecela amepigiwa simu na ndugu wa mtuhumiwa

baada ya taarifa za binti yao kusambaa katika mitandao ya kijamii, na kusema kuwa ni kweli kuwa ndugu yao amekamatwa ila si kweli kuwa amehukumiwa kunyongwa nchini Misri siku ya Ijumaa, Juni 7, 2013 kwani bado hata hajahukumiwa.

Inaelezwa pia kuwa ingawaje asili ya Fatma ni Tanzania, uraia wake ni wa Oman kwa mujibu wa pasipoti aliyokamatwa nayo.
Picture
(source: SalmaMsangi.com)
Picture
(source: SalmaMsangi.com)
Picture
(source: SalmaMsangi.com)

http://www.youtube.com/watch?v=vg19ZYsEhrA&feature=player_embedded

No comments:

Post a Comment