Sunday, May 19, 2013

VURUGU ZA MACHINGA IRINGA

Hili  ni  eneo la National moto  ukiwaka katikati ya  barabara

Maeneo ya Makorongoni yakiwa yametanda  moshi mzito
POlisi wakilinda barabara  ya Iringa - Dodoma ambayo  ilitekwa na  wamachinga hao na kuchoma mataili  barabarani

Wananchi  wakiwa  juu ya nyumba  zao  kushuhudia matukio


Hali bado  yaendelea  kwenda  kombo katika Manispaa ya  Iringa  baada  ya  askari  polisi kukamata  watu  zaidi ya 50 akiwemo  aliyekuwa mgombea udiwani kata ya Kwakilosa na kampeni  meneja  wa Chadema jimbo la Iringa mjini Abuu Majeck

Hadi  sasa biashara  katika mji mzima  zimesimama na polisi  wameendelea kuweka  sawa  ulinzi katika mitaa mbali mbali .

Kwa  sasa baadhi ya mitaa ya mji  wa Iringa imetanda  moshi  uliotokana na mataili  yaliyochomwa na machinga  hao.

Taarifa  za  sasa  kutoka jeshi la  polisi ni kwamba mbunge  wa  jimbo hilo mchungaji Peter Msigwa (Chadema) ambae anadaiwa  kuwa chanzo cha vurugu  hizo anasakwa  japo mtandao  huu nusu saa iliyopita  ulimshuhudia akiwa  eneo la chuo  cha Tumaini katika harambee  inayoendeshwa na waziri mkuu  wa zamani Mh. Sumaye .


Mbunge mchungaji  Peter Msigwa
Polisi  waliotoka  kumkamata  mbunge Msigwa  leo





Gari ya  mbunge Msigwa kabla ya  kukamatwa  leo kwa kuhusishwa na vurugu 
 
..........................................................................................


Na Francis Godwin, Iringa
MASAA  zaidi ya 6 ya mapambano kupiga  mabomu ya machozi na kurushiana  mawe kati ya wafanyabiashara  ndogo  ndogo (machinga ) na  askari  wa  kikosi cha  kutuliza  ghasia (FFU) mkoani Iringa  yaishia pabaya  kwa  jeshi la  polisi kumkamata  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  (chadema) na  watu  wengine zaidi ya 60
Polisi  watumia  mabom ya machozi  kutawanya machinga  wapiga mabomu hadi stendi kuu ya mabasi  abiria  walazimika  kutimua  mbinu na kuacha mizigo  yao katika magari   huku machinga  hao wakitumia mawe  na kuchoma mataili  moto barabarani  kuvunja vioo vya gari  la Zimamoto na kuharibu mali mbali mbali kama  njia ya  kupambana na  polisi
Tukio hilo la Mapambano  kati ya machinga na polisi lilitokea leo  kuanzia  muda wa saa 3  asubuhi  na kuendelea  hadi saa 8 mchana katika  eneo la Mashine  tatu  mjini  Iringa na maeneo mbali mbali ya mji  wa Iringa .
Mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com ambao ulikuwepo  eneo la  tukio  toka  saa 12  za asubuhi  ya jana  alishuhudia kundi kubwa la askari  wa FFU wakiwa na gari la maji ya  kuwasha ambao  wakesha wakilinda  eneo hilo .
Askari  huo  walilazimika  kukesha wakilinda eneo hilo  kufuatia  kauli ya  mbunge  Msigwa aliyoendelea  kuitoa katika  mikutano yake ya hadhara  mjini hapa  kuwhamasisha  machinga  hao ambao  Halmashauri ya Manispa ya  Iringa  iliwahamisha  eneo hilo la mashine tatu  na kuwapeleka  eneo la Mlandege kabla ya  mbunge Msigwa kuwahamasisha  kurejea  tena  eneo hilo.
Kabla ya  mbunge Msigwa  kufika  eneo hilo majira ya  saa 3 asubuhi machinga  hao ambao  walikuwa  wamejikusanya makundi madogo madogo   bila  kupanga  biadhaa zao  walisikika  wakidai  kumsubiri  mbunge Msigwa kama alivyopata  kuwaahidi  kuwa atafika  eneo hilo kuungana nao kwa  kuwa machinga  mpya  .
Hata  hivyo baada  ya mbunge  huyo kufika akiwa na gari lake  la kibunge  ambalo lilikuwa lilikokota tela  la  kuhifadhia mizigo  alisimama  eneo hilo na  kuendeleza msimamo  wake  wa kuwataka machinga  kupambana na baada ya  muda alitoweka  eneo hilo kabla ya  polisi  kuanza  kuwatawanya  machinga hao kwa mabomu ya machozi .
Wakizungumzia  hali hiyo  ambayo ni ya  kwanza kutokea katika  mji  wa Iringa wakazi  wa mji  wa Iringa  walisema  kuwa mbunge  na  viongozi  wengine  wa  serikali  wanapaswa  kulaumiwa kwa  kushindwa  kutumia njia nzuri ya  kukutana  kwa ajili ya kumaliza  mvutano huo  ambao unaendeshwa  kisiasa  zaidi.
Festo Sanga  alisema  kuwa  hali  ilipofikia  ni mbaya zaidi na  hivyo  busara  zinahitajika kwa ajili ya  kutatua  tatizo  hilo  ikiwa ni pamoja na kutazama  eneo zuri kwa ajili ya machinga  bila  kuendelea  kuonyeshana  ubabe .
Sanga  alisema  kuwa machafuko  yaliyojitokeza leo   ni machafuko ambayo wakazi  wa mji  wa Iringa  walikuwa  wakishuhudia katika  vyombo  vya habari  katika  mikoa  mingine  ukiacha  lile la Septemba 2 mwaka  jana lililotokea  kijiji  cha Nyololo kati ya  wafuasi  wa Chadema na polisi na kupelekea kifo cha aliyekuwa mwenyekiti  wa klabu  ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa marehemu Daud Mwangosi.
“Kweli katika hili  mbunge wetu hapaswi kuendelea  kulazimisha machinga  kuvunja  sheria  ila anayo nafasi ya  kukutana na viongozi  wenzake  ili  kutafuta  suluhu  ya jambo  hilo vinginevyo wanaoteseka  na machinga na  wale  waliokamatwa kwa  vurugu hizo  ujue  wengi  waliopigwa mabomu ya machozi si machinga  wengine  walikuwa  wasafiri na badhi yao  walikuwa  wakielekea makanisani ”
KUhusu  kukamatwa kwa mbunge  huyo na kuhojiwa na  polisi  juu ya vurugu  hizo Sanga  alisema kwa upande  wake analipongeza  jeshi la  polisi kwa  kutumia busara  zaidi  ya  kumkamata  mbunge   kama mhusika mkuu  na  kuliomba  jeshi la  polisi kuwaachia  wananchi  waliokamatwa  kwa  vurugu  hizo.
Huku  Sarah Kalinga  alidai  kuwa  chanazo cha machafuko hayo ni mvutano kati ya  CCM na Chadema na  kuwa  ilipaswa  vyama vyote  viwili  kukutana na  kuwasaidia  machinga  badala ya  kuwanyanyasa  kwa  kutumia nguvu  kuwabana .
Hata   hivyo  alisema wao kama walalahoi wanampongeza  mbunge wao kwa kuonyesha kuwapigania japo haungi mkono njia  inayotumiwa na mbunge ya  kuwahamasisha   kuvunja  sheria na kuwa  matatizo na majeraha  wanapata  wao  wananchi  na sio mbunge.
Awali  mbunge mchungaji Msigwa  kabla ya  kukamatawa na  jeshi la  polisi alitoweka katika mazingira  tata katika  eneo hilo la mashine  tatu na  kuibukia eneo la chuo  kikuu cha Tumaini Iringa ambako kulikuwa na harambee  ya  kuchangia Kanisa na mgeni  rasmi akiwa  waziri mkuu mstafu Frederick Sumaye na mara  baada ya  shughuli  hiyo  kumalizika ndipo alipokamatwa na polisi na kufikishwa  kituo cha  polisi.
Kabla ya  kukamatwa  kwake mbunge Msigwa alizungumza na mwandishi  wa habari hizi na kuwa  yupo tayari kukamatwa  wakati  wowote na  kuwa kamwe  ataendelea  na msimamo  wake  wa  kuwataka Machinga  kufanya  biashara  eneo hilo.
Mbali ya  kukamatwa  kwa  mbunge  Msigwa  kwa  kuhusishwa na vurugu  hizo pia  jeshi la  polisi  mkoani Iringa  linawashikilia  watu  wengine  zaidi ya 60 akiwemo  aliyekuwa kampeni meneja  wa Chadema  jimbo la Iringa mjini na mgombea  udiwani  kata ya  kwa Kilosa  Abuu Changawa Majeck.
Huku  idadi ya majeruhi  waliojeruhiwa kwa  kupigwa mawe na machinga na  badhi ya machinga  waliokamatwa kwa  vurugu  hizo pia wakijeruhiwa  vibaya  wakati  wakipambana na  polisi hao.
Taarifa  kutoka  jeshi  la polisi zilizothibitishwa na kamanda  wa polisi mkoa  wa Iringa Michael Kamuhanda  zinadai  kuwa  watu  zaidi ya 60 ndio  wamekamatwa  hadi  sasa na  jitihada za  kuwasaka wengine  waliohusika katika  vurugu  hizo ambazo zimesababisha uharibifu mkubwa wa mali  za  wananchi unaendelea.
Huku akidai  mali  mbali mbali  zimeharibiwa likiwemo gari  hilo la zimamoto mjini Iringa pamoja na uharibifu  mwingine  mdogo  mdogo  wa mali za  wananchi .
Jeshi  hilo la polisi  limesema kamwe halipo tayari  kumwachia mbunge Msigwa kwa leo hadi hapo atakapofikishwa mahakamani Kesho
MWISHO










 

Habari  ambazo zimetua  hivi punde katika mtandao huu  zinadai kuwa msafara  wa askari  wa FFU  pamoja na gari la zimamoto  kutoka  jiji la Mbeya  upo njiani  kuja  mjini Iringa  kuongeza nguvu  zaidi .

mbunge Msigwa (kulia)akizungumza na msaidizi  wa askofu  wa KKKT dayosisi ya Iringa
Mbunge Msigwa akisalimia katika harambee  iliyoendeshwa na Sumaye leo katika  chuo  cha Tumaini Iringa

Watalii  wakiogopa kuendelea na  safari  baada ya  kutokea machafuko mjini Iringa

Jeshi la  polisi  mkoa  wa Iringa  limemkamata  mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (Chadema) kufuatia  kuhusishwa na vurugu  za machinga eneo la mashine tatu hii leo

Hivi  sasa  mbunge  huyo yupo katika  kituo kikuu  cha polisi mjini Iringa akihojiwa na polisi kufuatia vurugu  hizo ambazo kwa  sasa  zimetulia na  wananchi  wameanza  kuendelea na biashara  zao.

No comments:

Post a Comment