"SERIKALI dhalimu huondolewa na wenye hasira na waliochoka, kunyanyaswa na kudhulumiwa haki zao".
Hayo
yamesemwa na Mbunge wa Singida Mashariki na mnadhimu mkuu wa kambi ya
upinzani bungeni Tundu Lissu katika mkutano wa hadhara uliomalizika hivi
punde katika viwanja vya Mkwawa nje kidogo na geti la Chuo Kikuu.
Lissu
amesema serikali yoyote haiondolewi madarakani kwa maombi bali kwa
kutumia maamuzi ya kisiasa na kwa kupiga kura za kuikataa hasa unapofika
wakati wa kufanya uchaguzi.
Amesema
mambo ya kikaisari yanatatuliwa kikaisari na hali lilipofikia taifa la
Tanzania, ni pabaya ambapo wananchi wana kila sababu ya kukichukia chama
tawala ambacho kinawatia umasikini wananchi bila sababu.
"Usije
ukadanganyika kuwa ukimuomba Mungu utakuta CCM imetoka madarakani, haya
ni mambo ya kikaisari ambayo yanatakiwa kutatuliwa kikaisali hivyohivyo.
Usidhani ukimuomba Mungu pale utakapokuwa unamaliza sala utakuta CCM
haipo, kamwe! Huu ni wakati wa kuichukia na kuiondoa, haifai tena. Ila
siwaambii kama musiende kumuomba Mungu, saline lakini hakikiseheni
mnachukua maamuzi ya kuiondoa CCM" amesema Lissu.
Amesema
upinzani wamekuwa na hoja za kuisaidia serikali lakini kwa sababu ya
ufinyu wa fikra za viongozi wa chama hicho, hoja zao zimekuwa zikipuuzwa
kwa sababu ya uwingi wa watu kwa kutumia "ndiyooo!" badala ya kuangalia
mwenendo mzima wa maisha ya watanzania.
"Ndugu
zangu, kwenye bunge letu tuna wabunge wachache tu na wengine wengi ni
kundi tu la walaji ambalo halina kazi yoyote" amesema.
Amesema CCM imegombana na kila mtanzania kwa kila nyanja kwa kuwa kila kitu kinachofanyika na serikali kinambana mwananchi.
Ameeleza
kuwa serikali imeingia katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kutumia hela
za watanzania bila sababu huku ikiwanyima haki zao pale wanapostaafu.
"Kila
kinachofanyika na serikali kinatumia pesa za wananchi wanaoweka pesa zao
katika mifuko yao bila kuwaarufu wananchi wenyewe. Niwambieni kuwa leo
hii kwa wewe unayeweka pesa zako katika mfuko wowote wa jamii pindi
utakapostaafu imekula kwako hutaipata tena pesa yako kwa sababu watu
wamegawana" amesema.
Amesema
hakuna ambaye halalamiki juu ya kile anachotendewa na serikali awe
polisi, mwalimu, machinga, mama lishe hata mwanafunzi.
Hata
hivyo amesema jeshi la polisi linalotumika na baadhi ya wanasiasa wa
Chama cha Mapinduzi limedhurumiwa na serikali kuliko hata machinga.
Akifafanua
zaidi amesema kila wakati zimekuwa zikitolewa pesa kwa ajili ya mafunzo
ya jeshi la polisi, nyongeza za mishahara, likizo na kupandishwa vyeo
lakini zimekuwa zikipigwa juu kwa juu na viongozi wa chama tawala.
"Leo hii
ugomvi wa wanafunzi wa vyuo vikuu na serikali ni mkopo, nchi inadaiwa na
benki za nje, taasisi za fedha za nje na mashirika ya fedha, walimu na
polisi pia; ni nani hajaumizwa na serikali hii dhalimu?" amesema.
Amewataka
watanzania kupongezana kwa kazi ambayo imekwisha kufanyika na
kuwakumbusha kuwa bado kuna kazi kubwa ipo mbele yao kuhakikisha
serikali dhalimu inaondoka.
Lissu
amekwenda kinyume na kauli ya Waziri William Lukuvi bungeni kuwa kamanda
wa polisi Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda anafanya kazi nzuri na hivyo
kumtaka aendelee na kazi hiyo kuwa inaonesha dhahiri jinsi Chama cha
Mapinduzi kinavyotumia jeshi la polisi kuwakandamiza wananchi.
"Katika
tume zilizoundwa kuchunguza mauaji ya mwandishi wa habari Daudi Mwangosi
ikiwemo tume ya serikali ya tume ya haki za binadamu, ripoti inasema
Kamuhanda Mwangosi aliuawa kwa usimamizi wa Kamuhanda na ni muuaji
lakini leo hii anasimama Waziri halafu anasema Kamuhanda huyo huyo
anafanya kazi nzuri! Inatisha sana" anasema.
Hata
hivyo amesema Kikwete pamoja chama chake wanatambua kuwa inchi ilipofika
sasa mbele ni giza tu kwa kuwa hakuna njia zinazowezakutumika
kuwakomboa wananchi kwa udhalimu wao.
Lissu
amesema wananchi wa hali ya chini ndiyo wanaokamuliwa kodi huku watoto
wa viongozi na wafanyabiashara wakubwa wakiachwa kwa sababu ndio
walioinunua serikali.
Hata
hivyo mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) Olime Mwakilembe amesema
imefika mahali CCM inakata ushauri na kufanya mambo magumu kwa njia
rahisi wakidhani wanatatua matatizo na badala yake kuwapa mzigo
wananchi.
Amesema
hali ya maisha ya watu ilipofika inatisha kwa sababu ya serikali
legelege isiyo na masikio inayotumia mabavu kuwalazimisha wananchi
kuingia motoni badala ya kutumia rasilimali watu kuokoa maisha ya
watanzania.
"Matatizo
magumu wanafanya kwa njia rahisi. Ushauri wa maana wanaukata kwa sababu
ya uhuni wao wa kutumia mabavu na kuwanyanyasa wananchi ambao ndio
walipa kodi wanazoendeshea maisha yao na familia zao. Uhuni huu
unafanyika kwa wazi kabisa huku watanzania wakiuona" amesmea.
Amewataka
watanzani kutokufumbia mamcho matatizo yanapotokea ambayo chanzo kikuu
ni viongozi wanafiki waliojaa dhuruma na kujilimbikizia mali.
Hata hivyo amesema wakati wa kuiaga CCM umefika na kiama chake kimekamilika ambacho ni Chadema.
Mkutano
huo uliandaliwa na shirikisho la vyuo vikuu Mkoa wa Iringa ambavyo ni
Chuo Kikuu kishiriki cha Tumaini Iringa, Chuo Kikuu kishiriki cha Mkwawa
na Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO).
Mwenyekiti
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa Jimbo la
Hai, Freeman Mbowe akimkabidhi nahodha wa Timu ya Mpira wa Miguu ya
Wazawa FC ya KIA, Efati Mwasumbi, zawadi ya jezi na mipira kwa ajili ya
timu hiyo jana. Katikati ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la chama
hicho (BAVICHA) Dorice Cornel. Kiongozi huyo yuko katika ziara ya wiki
mbili jimboni kwake kuzungumza na wananchi wa jimbo hilo.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman
Mbowe na Mbunge wa Hai, akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa chama hicho
Kijiji cha Mtakuja, Mzee Ally Mbatia. Mbowe yuko katika ziara ya kukagua
uhai na kuimarisha ujenzi wa chama katika ngazi ya chini kabisa ya
chama hicho, msingi, kwenye maeneo ya vitongoji mbalimbali katika vijiji
vya Jimbo la Hai.
No comments:
Post a Comment