HUU
ni msimu wa parachichi kwa Ukanda wa Pwani, kama yalivyo matunda yote
kwa ujumla kuwa yana faida sana katika mwili wa binadamu, vivyo hivyo na
parachichi. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kupambana na maradhi hatari
ya moyo na sataratani ya matiti kutokana na virutubisho ilivyonavyo.
Kwa
mujibu wa utafiti wa kisayansi juu ya tunda hili, lina kirutubisho aina
ya Aloic Acid ambayo ni aina fulani ya mafuta mazuri yanayosaidia
kushusha kolestro mwilini. Katika utafiti mmoja waliofanyiwa watu kadhaa
waliokuwa na matatizo ya kolestro mwilini, baada ya kutumia parachichi
kwa muda wa siku saba, walionesha mabadiliko mazuri katika afya zao kwa
kupungua kiwango cha kolestro mbaya mwilini.
Aidha, parachichi lina
kiwango kikubwa sana cha madini aina ya ‘potasium’ ambayo ni muhimu sana
katika kuimarisha mzunguruko wa damu mwilini. Inaelezwa kwamba ulaji wa
kiwango kikubwa cha madini ya potasiam, hutoa kinga madhubuti dhidi ya
magonjwa yatokanayo na mzunguruko mbaya wa damu mwilini, kama vile
ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu na kiharusi.
Mbali ya madini hayo,
parachichi lina virutubisho vingine kama vile Folate (Folic acid)
ambacho ni muhimu sana kwa afya na ustawi wa moyo, kwa maana hiyo watu
ambao wanakula sana vyakula kama parachichi lenye kirutubisho hicho,
watukuwa salama dhidi ya magonjwa ya moyo au kiharusi kwa asilini 55.
Virutubisho
vingine vinavyopatikana kwa wingi kwenye parachichi ni Fatty Acids,
ikiwemo Oleic Acid. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni, imedhihirika
kwamba virutubisho hivyo ni kinga tosha dhidi ya saratani ya matiti.
Kwa maana nyingine, wanawake wanaokula kwa wingi maparachichi, wanaipa
miili yao kinga dhidi ya saratatani hiyo ambayo hivi sasa imekuwa tishio
miongoni mwa wamawake wengi nchini.
Parachichi
linaweza kuliwa kama mtu atakavyopenda, wapo watu wanaopenda kula bila
kuchanganya na kitu kingine, lakini pia parachichi linaweza kuliwa kwa
kupaka kwenye mkatate badala ya Blue Band. Halikadhalika parachichi
linaweza kuliwa kwa kuchanganya na nyanya, vitunguu, ndimu na chumvi
kidogo kama kachumbari ya kipekee au kunywa juisi yake.
VIRUTUBISHO VYA PARACHICHI
Kwa ujumla, parachichi ni chanzo kizuri
cha Vitamini K, Vitamini B6 na Vitamini C. Aidha tunda hili lina
kiwango kizuri cha virutubisho aina ya Folate, kopa na kambalishe
(Fiber). Fiber ni muhimu katika kuwezesha mtu kupata choo laini na bila
matatizo. Bila kusahau kwamba tunda hili ni chanzo kizuri pia cha madini
ya potasiam. Lina kiwango kikubwa kuliko hata ndizi.
Ingawa
parachichi ni tunda, lakini lina kiwango kikubwa cha mafuta (fats)
ambayo yanakadiriwa kuwa kati ya asilimia 71 – 88, kiwango ambacho ni
cha juu kwa silimia 20 ukilinganisha na matunda mengine. Kwa wastani,
parachichi moja lina gramu 30 za mafuta, lakini kati ya hizo, gramu 20
ni za mafuta mazuri kiafya (Monounsaturated fats na Aloic Acid) ambayo
husaidia kujenga afya bora mwilini.
Utafiti zaidi kuhusu tunda hili
unamalizia kwa kusema kwamba parachichi lina takribani aina 20 za
Vitamin, madini na virutubisho muhimu (Phytonutriens) ambavyo hutuo
kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mengi hatari. Baadhi ya Vitamini
zilizomo na asilimia zake kwenye mabano ni pamoja na Vitamin E (4%),
Vitamin C (4%), Folate (6%), Fiber (4%), Iron (2%) na Potasium (4%).
Kwa faida hizo na huu ni msimu wa parachichi (avocado), umeshakula mangapi hadi sasa?
Toka: GPL
No comments:
Post a Comment