Thursday, May 16, 2013

TOHARA INAPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU


tohara fed4e

Mratibu wa mapambano dhidi ya UKIMWI wilaya ya Makete mkoa wa Njombe, Dkt. Shadrack Sanga

Imeelezwa kuwa wanaume waliofanyiwa tohara si kweli kwamba hawatapata virusi vya Ukimwi na badala yake kutawasaidia kupunguza uwezekano wa kupata vvu kwa asilimia 60.

 Hayo yamesemwa na mratibu wa Ukimwi wilaya ya Makete(DAC) Dkt. Shadrack Sanga(pichani) wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu umuhimu wa tohara ya wanaume wilayani hapo
 Amesema kumekuwa na taarifa zilizozagaa kuwa mwanaume akishafanyiwa tohara hawezi kupata vvu ambapoa amesema taarifa hizo si za kweli na ukweli ni kwamba mwanaume huyo atapunguza asilimia 60 za kupata vvu kuliko yule ambaye hajatahiriwa
 ”Naomba hili lieleweke wazi, mwanaume ambaye hajafanyiwa tohara na yule aliyefanyiwa wote wanaweza kupata vvu, lakini aliyefanyiwa tohara anaupungufu wa asilimia 60 kupata vvu lakini si kwamba hatapata” alisema
 Katika hatua nyingine Dkt. Sanga amesema tangu kampeni ya tohara ya wanaume maarufu kama dondosha mkono sweta ianze rasmi wilayani Makete mwaka 2011 jumla ya wanaume 9,669 wamefanyiwa tohara
 Amesema muitikio ni mzuri lakini bado idadi ya wanaume ambao hawajafanyiwa tohara ni kubwa hivyo anatoa wito kwa wanaume kuacha woga na aibu ya kwenda kufanyiwa tohara ambayo ianatolewa bure
 Hivi sasa mkoa wa Njombe unaongoza kitaifa kwa kuwa na maambukizi makubwa ya virusi vya Ukimwi, ambapo imegundulika kuwa wanaume wengi wa mkoa huo kutofanyiwa tohara ni miongoni mwa sababu kubwa zinazopelekea maambukizi hayo kuwa juu. Chanzo: Edwin Moshi

No comments:

Post a Comment