Wednesday, May 15, 2013

MBINU MPYA YA KUANDAMANA KENYA

Hii mbinu ya kutanguliza kiti moto kwenye maandamano huko nchini Kenya nimeipenda sana, sijui maustadhi askari walisogea au la?

Nchini Kenya hii leo tarehe 14.05.2013 kunafanyika maandamano ya amani ya kupinga nyongeza ya mishahara ya wabunge.
Wabunge nchini Kenya wadai nyongeza ya mshahara

Wabunge nchini humo wanataka tume inayoshughulikia mishahara ya watumishi wa umma iongeze mishahara yao kutoka elfu 532,000 hadi 850,000. Wabunge hao wa Kenya wanasema kima walichoekewa ni kidogo sana kukidhi mahitaji yao.
Hata hivyo tume hiyo imesema haitabadilisha msimamo wake huku ikitupilia mbali vitisho kutoka kwa wabunge hao waliosema wataifuta kazi tume hiyo iwapo matakwa yao hayataridhiwa.
Mwandishi wetu wa Nairobi Reuben Kyama yuko katika maandamano na kwanza anatueleza hali ilivyo kwa sasa.
Mwandishi Amina Abubakar
Mhariri Yusuf Saumu

No comments:

Post a Comment