Serikali za
Uganda na Rwanda kwa kushirikiana na shirika la kuwahudumia wakimbizi la
UNHCR, zinapanga kuwarejesha nyumbani wakimbizi kutoka Rwanda katika
kipindi cha miezi miwili kutoka sasa. Hii
ni kwa wale ambao wameishi ukimbizini Uganda kwa karibu miongo miwili,
hata hivyo sio wote wanaridhia kurejeshwa kwao kwa hiari nyumbani.
Baadhi
wanadai kuwa ingawa wao hawapaswi kurejeshwa lakini wanashanga kuona
majina yao yameorodheshwa miongoni mwa wanaotaka kurejea.
Hata hivyo madai hayo yamekanushwa na maafisa wanaoshughulikia wakimbizi wa Uganda.
Mwisho wa
mwezi Juni mwaka huu, ndio muda uliopewa wakimbizi kutoka Rwanda kuwa
wanapoteza hifadhi ya ukimbizi ikitolewa hoja kuwa kwa sasa nchi yao ni
tulivu na amani.
Serikali ya
Rwanda imekuwa ikiomba shirika la wakimbizi kufuta kipengee
kinachowasaidia raia wa Rwanda wanaoishi nje ya nchi hiyo kama
wakimbizi.
Kipengee
hicho kinawahusu wakimbizi wa Rwanda kutoka miaka ya 1950,
1970,waliokimbia mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 na pia kuzorota kwa
usalama kabla ya mwaka wa 1998, na wakuu Uganda wanasema wanyarwanda
wanaokumbwa na kipengee hicho wanafikia elfu nne.
Hata hivyo
kuna wanaodai kuwa walitoroka Rwanda kwa usalama wao baada ya mwaka wa
1998 wanaodai kuwa majina yao yameorodheshwa katika wale wanaopaswa
kurejea nyumbani.
Lakini
kamishna wa wakimbizi katika ofisi ya waziri mkuu inayohusika na
wakimbizi David Kazungu amepinga madai kuwa majina ya wakimbizi
waliokuja baada ya 1998 pia yameorodheshwa.
''Hiyo si
kweli na hakikisha kabisa kuwa huo ni uongo.Hii ni kwa sababu
tunategemea habari za uhakiki mbalimbali tuliofanya na shirika la
UNHCR.Hawa watu wakija husajiliwa rasmi na kila mwaka tunahakiki majina
ya wakimbizi hao,'' alisema bwana Kazungu
''Lakini
ikiwa umehakikiwa mara kadhaa tangu uwasili na kila mara mwaka wako wa
kuwasili ni 1997 kwanini mara moja unabadili mwaka wa 1999 au 2000?
Haiwezekani kuwa ulikuja mwaka wa 2000 na tukuweka katika data zetu kama
aliekuja mwaka wa 1997 data zetu hazikubali hiyo,'' aliongeza kusema
Kazungu
Ukiacha hayo wakimbizi wengi kutoka Rwanda wanaogopa tarehe ya Julai 31 mwaka huu.
Juni 31 ni
siku imepangwa kufuta kipengee cha wakimbizi lakini utekelezaji wa hatua
hiyo haumanishi kuwa ghafla bin vuu wakimbizi hawataingia tena.
Wahusika
wataarifiwa ikiwa wao ni waathirika na tarehe hii ikiwa walikuja Uganda
kabla ya 1998.Kisaha watachunguzwa ikiwa wana sababu sababu halali ya
kutorejea nyumbani kwa hiari, na endapo jopo litaaamini hoja zako
utaendelea kubaki mkimbizi na utasaidiwa vilivyo. Lakini mbali na hili
maafisa wanawahimiza wakimbizi kurejea Rwanda.
Wakimbizi
halisi kutoka Rwanda ambao wako katika orodha ya kurejeshwa nyumbani
baada ya Juni 31 wanafikia 4,100, ingawa duru Fulani zilikuwa zimedai
kuwa wanazidi elf 8.
Chanzo - BBC Swahili
No comments:
Post a Comment