BAADA
ya hivi karibuni Mtangazaji wa Radio Times, Khadija Shaibu ‘Dida’
kufunga ndoa na mwanaume aitwaye Ezden, mashosti zake wamemtaka kutulia
sasa na asijaribu kugeuza ndoa kuwa fasheni. Wakizungumza
na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya mastaa walioomba hifadhi ya
majina yao ambao walihudhuria ndoa hiyo iliyofungwa Ijumaa iliyopita
Ubungo jijini Dar walisema, wamechoka na mialiko ya ndoa zake kila baada
ya kipindi kifupi hivyo ni wakati sasa wa kutulia, Hii ni ndoa ya Tatu ya Dida.
“Asifanye
ndoa kama fasheni, tumechoka kuhudhuria sherehe za ndoa yake, kama ana
kasoro, ajirekebishe ili atulie sasa ajenge maisha yake,” alisema staa
mmoja ambaye ni rafiki wa karibu na ndugu wa Dida. Hata hivyo, akizungumzia kuhusu kuolewa huko, Dida alisema safari hii ndoa yake ikivunjika haolewi tena.
Kwa hisani ya Na Hamida Hassan /GPL
No comments:
Post a Comment