Mmoja kati ya watuhumiwa wa wizi Mafinga wilaya ya Mufindi akiwa amechezea kichapo toka kwa wananchi wenye hasira kali leo |
Askari polisi wakisaidia kuokoa maisha na watuhumiwa wa upigaji nondo Mafinga |
Watuhumiwa hao wakiwa kituo cha polisi baada ya kuokolewa kutoka mikononi mwa wananchi wenye hasira kali leo |
Watu watatu wamenusurika kufa baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kugundulika kuwa ni vibaka ambao hupiga nondo na pengine kuwachoma visu raia/wananchi warudipo majumbani mwao nyakati za usiku.
Watu hao walikamatwa juzi hapa Mafinga na watu wa stand kuu ya mabasi, na msako wa kuwakamata vibaka hao ulikuwa ni wa kundi kubwa kutoka standi na kuwafuata kinyanambo sehemu za vilabu vya pombe za kienyeji ambapo mara ya kwanza walipoenda walimkuta mmoja na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya standi kuu, alipobanwa aoneshe wezake akataja maeneo ambayo huwa wanashinda na alipoelekeza tu hilo eneo jopu nzima la watu wa standi wakarudi tena huko Kinyanambo na kuwabamba vibaka wawili tena. Hivyo vibaka hao hadi leo hii bado wameshikiliwa mikononi mwa polisi kwa uchunguzi zaidi. Picha na Rogers Mselu
No comments:
Post a Comment