Thursday, September 5, 2013

MWENGE WA UHURU UPO DSM SASA

Picture_398_054e6.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuuwa Chama cha Skauti Tanzania Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Picture_324_6daab.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuuwa Chama cha Skauti Tanzania Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.(P.T)
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai akitoa salamu za shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajati Mwantum Mahiza (aliyevaa Miwani) kabla ya kuukabithi Mwenge huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo(kushoto) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa, katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Picture_402_a4f95.jpg
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Terminal one.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

No comments:

Post a Comment