


Meza yetu ya habari imepokea habari toka Kariakoo zikitujuza Uvamizi wa gafla
uliofanywa kwa kushirikisha Polisi na
Raia wa Kizungu waliopita kwenye maduka na kuchukua simu zote za aina ya Samsung za kichina.
Baada ya kufanya mahojiano kwa njia ya mtandao na simu na baadhi
ya wafanyabiashara, tulifahamishwa kuwa hii ni mara ya tatu na baadhi ya
wafanyabiashara wamekiri kuwa huu ni mchezo mchafu unaochezwa na baadhi ya Maaskali polisi wa
Kituo cha Msimbazi......"
Kwa masharti ya kutotajwa jina
mfanyabiashara mmoja alikuwa na haya ya kusema “yaani hawa wazungu wamevamia hapa na Askari na kuchukua simu za kichina za
Samsung wakati sisi mzigo tunanunua china hivi ni halali kweli ? Ujue Watanzania tunashushana
na kutiana umaskini wenyewe kwa wenyewe ... hii ni mara ya tatu na kila wakija
wanachukua mzigo wote hivi ni kweli
serikali haijui ? au mpaka siku
tuliwashe ndio watu watafutane au ijulikane? Au wanataka waseme tulianzisha
vurugu , Raia wa kigeni aingie duka la mzalendo kupekua kweli jaman? Inauma
sana unajua dada ?
No comments:
Post a Comment