Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara
(kulia) akimkabidhi Bendera ya Taifa,Redd's Miss Tanzania
2012/13,Brigitte Alfred (katikati) anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni
kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss
World 2013).Kushoto ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole
Naiko.
Mkurugenzi
Mkuu wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa
Shindano la Miss Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania
2012/13,Brigitte Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya
Taifa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella
Mukangara (kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya
kumuaga Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es
Salaam usiku huu.
Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa
pili kulia) akitoa nasaha zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's
Miss Tanzania 2013,wakati wa hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu
ya kumuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto)
anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki
Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku
huu kwenye Hoteli ya Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia
ni Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto
ni Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
Redd's
Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa
hafla hiyo ya kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya
Giraffe,jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment