Monday, May 6, 2013

WAKALI WA MIC, DIAMOND MUSICA WAFUNIKA DAR LIVE


Washiriki  wa The Mic King wanaowania gari jipya aina ya Fun Cargo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mmoja wa Wakali wa Mic akimwaga mistari kwa mashabiki.…
Washiriki  wa The Mic King wanaowania gari jipya aina ya Fun Cargo wakiwa katika picha ya pamoja.
Mmoja wa Wakali wa Mic akimwaga mistari kwa mashabiki.
Lusajo Jackson akichana verse za Mabaga Fresh.
...Mchuano ukiendelea.
Martin Fundi akionyesha mbwembwe zake stejini.
Boniface Milumbe akiwa kazini.
Shindano likiwa limepamba moto.
Majaji wakiwa kazini.
Diamond Musica wakishusha burudani.
WAKALI wa muziki wa hip hop wanaochuana ndani ya Ukumbi wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam pamoja na Bendi ya Diamond Musica ‘Original’ jana walifanya kufuru ya burudani ukumbini hapo.
Wakali wa hip hop wanaochuana kuwania gari jipya aina ya Fun Cargo ‘New Model’ wakiwa wanaelekea ukingoni mwa fainali za kipute chao cha The Mic King kinachotarajiwa kufanyika Mei 25 mwaka huu kila mmoja ameonesha nia ya kutaka kulitwaa gari hilo.
Washiriki kumi waliosalia kwenye kipute hicho wiki hii walikuwa na kazi ya kuonesha uwezo wao kuchana mistari ya wanahip hop iliyowahi kubamba katika ‘gem’.
Wakali hao walichana kiusawia mistari ya wasanii mbalimbali iliyowahi kutamba ikiwemo ya Profesa J na Mabaga Fresh ambapo wasanii hao waliwapagawisha mashabiki na kupiga bonge la shoo na kuonekana kama kuwafunika wakongwe hao.
Majaji wa mpambano huo, Abby Cool, DJ John Dilinga JD na Ally Baucha waliumiza vichwa kuchambua uwezo wa wakali hao ambapo waliishia kumwaga sifa.
Baada ya wakali hao kushuka jukwaa Bendi ya Diamond Musica ambayo inatisha katika anga la muziki kwa siku za hivi karibuni ilivamia jukwaa na kupiga shoo ya nguvu iliyowachagiza mashabiki na kuwafanya wavamie jukwaa.
Bendi hiyo iliwatumia wanamuziki wake wapya na wakongwe na kupiga vibao vyao mbalimbali ikiwemo vipya na vya zamani.

No comments:

Post a Comment