eshi la polisi limekumbwa na kashfa
nyingine baada ya askari wake kudaiwa kumpiga risasi msichana wa miaka
16 baada ya kumkuta akivunja amri ya sita ndani ya gari.
Msichana huyo (Jina tunalihifadhi)
alikumbana na mkasa huo Jumatano usiku eneo la Mbagala Zakhem jijini Dar
es Salaam, ambapo alipigwa risasi sehemu ya makalio wakati akijaribu
kuwakimbia polisi kwa kutumia gari la mpenzi wake.
Mpenzi huyo (jina linahifadhiwa), alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi ya ubakaji.
Akizungumza na NIPASHE Jumapili jana
katika wodi ya Hospitali ya Temeke alikolazwa, msichana huyo alisema
siku ya tukio alikutana na kijana huyo majira ya saa 8:00 usiku katika
baa moja inayoitwa Kindau na kukubaliana kwenda kushiriki tendo la ndoa
kwa malipo ya Sh 20,000.
Alisema kutokana na muda huo kuwa usiku
sana hawakuweza kwenda katika nyumba ya kulala wageni na badala yake
walikwenda eneo la Zakhem na kisha walipaki gari kwenye uchochoro na
baadae walianza kubanjua amri ya sita.
Wakiwa kwenye kilele cha mapenzi yao, ghafla walishtukia gari la polisi likiwajia kwa kasi kwa nia ya kuwakamata.
“Tuliagana anilipe elfu ishirini wala
hakunibaka kama anavyodai, wao polisi walitukuta tayari tunamaliza
lakini kutokana na woga tulikimbia ili tusikamatwe,” alisema msichana
huyo.
Alisema wakati wanakimbia kwa kutumia
gari la mpenzi wake askari mmoja alifyatua risasi iliyopenya kwenye taa
ya gari na kwenda kumjeruhi sehemu ya makalio yake.
“Nilisikia mlio mkubwa wa bunduki, ghafla nilihisi kitu kimeingia mwilini mwangu na kuishiwa nguvu,” alisema kwa uchungu.
Alisema kwa kuona hali hiyo, mpenzi wake
alisimamisha gari kwa kujisalimisha na polisi walipowafikia walimtaka
mpenzi wake huyo atoe pesa kama malipo ya kitendo chao cha kukutwa
wakifanya mapenzi ama sivyo watampeleka kituoni.
Alieleza kuwa mpenzi wake hakuweza kutoa
pesa hizo ndipo walipoamua kumpiga na kumpeleka kituo cha polisi cha
Mbagala na yeye alifikishwa hospitalini hapo kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo, ndugu na jamaa wa mpenzi
wake wanapinga hatua ya polisi hao kutumia nguvu kubwa kama watu hao
walikuwa watuhumiwa wa ujambazi.
Wakizungumza wakiwa kwenye kituo cha
Polisi cha Mbagala kufuatilia hatma ya ndugu yao, ndugu hao ambao
hawakutaka majina yao yatajwe gazetini walisema hatua ya polisi kupiga
risasi huku wakitambua watu hao sio majambazi ni kitendo cha kinyama.
“Tunachoshangaa ni kwa nini polisi
wapige risasi wakati wakijua hawakuwa majambazi ila walikuwa wakifanya
mapenzi, hata hilo jalada la kesi walilofungua wanataka kuficha maovu
yao na sio vinginevyo,” alisema ndugu mmoja ambaye alijitambulisha kuwa
shemeji yake.
Alisema kimsingi tukio hilo lilikwenda
katika makubaliano yao na sio ubakaji kama wanavyodai, ila
kinachofanyika kwa sasa ni kutaka kumlinda askari mwenzao aliyejeruhi
kwa risasi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Temeke,
David Misime, alipopigiwa simu kuelezea tukio hilo, alisema kwa sasa
hawezi kulizungumza kwa kuwa yupo nje ya Mkoa kikazi.
No comments:
Post a Comment