Friday, May 3, 2013

MORINHO KOCHA MPYA CHELSEA

c 1ffda
Mourinho Kocha mpya Chelsea, amalizana na Abramovich London

c1 ff20a
Roman Abramovich ameripotiwa kukubali dili la kumrejesha Mourinhio Stamford Bridge.


c2 99d9f
Mgahawa wa Kitaliano wa La Famiglia in Chelsea.

KOCHA Jose Mourinho amekubali dili la kujiunga tena na Chelsea na atarajea rasmi Stamford Bridge Julai 1, kwa mujibu wa taarifa jana usiku.

Kocha huyo wa Real Madrid inadaiwa kupata chakula cha jioni na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich katika mgahawa wa La Famiglia Magharibi mwa London ambako inasemekana amekubali ofa ya mshahara wa Pauni Milioni 10 kwa mwaka, ingawa bado kunahitajika mjadala wa kuruhusiwa kuondoka Real. Abramovich atatakiwa kuilipa Real Pauni Milioni 12.

Chelsea itatangaza dili hilo kabla ya kwenda kwenye ziara yao ya kujiandaa na msmu mpya, Mashariki ya Mbali, ambayo inamaanisha kwamba mechi ya kwanza ya kurejea kwa Mourinho itakuwa ya kirafiki dhidi ya Singha All Stars XI nchini Thailand Julai 17.

Msaidizi wa zamani wa Mourinho, Andre Villas-Boas, Alhamisi alisema anafikiri dili hilo la kumrejesha bosi wake wa zamani katika klabu hiyo aliyopata nayo mafanikio limefanikiwa. 

Kocha huyo anayeinoa Spurs kwa sasa, ambaye alifanya chini ya Mourinho katika klabu za Porto, Chelsea na Inter Milan, alisema hawezi kuzungumza na swahiba wake huyo juu ya kuondoka Madrid na kurejea Ligi Kuu England hadi atamke rasmi kurejea kwake.

"Nina uhakika kiasi cha kutosha uamuzi umekwishachukuliwa,"alisema Mreno mwenzake huyo.

Inasemekana kwamba anafurahi kurejea England na Chelsea ni moja ya klabu zinazosaka kocha inaonekana sana, kwa kiasi kikubwa sana atatua huko. Chanzo: binzubeiry.

No comments:

Post a Comment