Thursday, May 16, 2013

MCHUNGAJI MSIGWA AWATAKA MACHINGA KUFANYA KAZI KWA UHURU

msigwa1 5842aMbunge  wa  jimbo la Iringa mjini akiwahutubia umati mkubwa wa wananchi  wa  jimbo hilo jioni ya leo katika eneo la stendi kuu ya mabasi ya mikoanimsigwa2 d46e7
Umati   wa  wananchi  wakimsikiliza mbunge  wao wa  jimbo la Iringa mjini
Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa amewataka  wafanyabiashara  ndogo ndogo (machinga ) mjini Iringa  kuendelea  kufanya kazi katika  eneo la Mashine  tatu  bila  kufanya  vurugu  zozote kwa  wale wanaozuia kufanya  hivyo.

Akizungumzia  suala la Machinga  kuendelea  kunyanyasika  mbunge Msigwa amesema  kuwa tayari suala  hilo ameanza  kulipigania bungeni  kwa waziri  mwenye dhamana  hivyo kamwe  machinga  Iringa  wasikubali  kunyanyasika .

Aidha mbunge  huyo amemtaka  katibu mkuu  wa chama  cha mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana  kutosubiri muda  wa  siku  21 alizozitoa  kumfikisha mahakamani kuwa  yupo tayari  kwenda mahakamani hata kesho.
Mbunge Msigwa amesema kuwa katika  ukweli kama  hata  kuwa tayari kumwogopa mtu na kuwa siku  zote atasimama katika  ukweli katika  kupigania maslahi ya Taifa  hili.

Mbunge  Msigwa amesema  kuwa hatua ya katibu mkuu  wa CCM kukimbilia katika  vyombo  vya habari  kutishia  kumfikisha mahakamani bila yeye mhusika  kupelekewa taarifa  ni  sawa na kumwogopa na  hivyo suala la Kinana kwenda Mahakamani  si  sawa ni  kumtishia nyau mtu mzima.

Kwani  alisema  kuwa  Chadema  ina  mawakili  waliojitosheleza na  kuwa hawatanyamaza kusema  ukweli kwa  kuogopa vitisho vyovyote. Chanzo: matukiodaima.com

No comments:

Post a Comment