Friday, May 17, 2013

MADRID WALALA 2-1 KWA ATRETICO

madrid2 4196a

Cristiano Ronaldo, baada ya kumfanyia madhambi Gabi



madrid3 74e28

Ronaldo akifunga bao



madrid4 3bf7f

Ronaldo alikuwa wa kwanza kufunga bao la kuongeza katika dakika ya 55 na baadaye Diego Costa aliisawazishia Atletico Madrid akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na nyota anayewindwa na Mmiliki wa Chelsea ,Roman Abramovich ili amsajili msimu ujao, Radamel Garsia Zarate Falcao.



madrid d5ff8

Joao Miranda akitia kambani bao la pili na la ushindi kwa Atletico Madrid watoto wa mjini wanasema amepiga ndosi ya maana kuzamisha gozi kambani, si mchezo hiyo ndio kazi
Na Baraka Mpenja
Mtangazaji wa mpira wa miguu utawasikia kwa maneno kama haya, “dakika zilizobaki ni ngumu kuzitaja!, tunamuangalia mwamuzi tu!, ni nafasi ya mwisho kwa Real Madrid, wakishindwa kufunga basi ndio hivyo wamekwenda na maji!.

 Nini pale?  Kocha Mourinho anazozana na mwamuzi pale, mwamuzi anasemaje”, heeee! kadi nyekundu! Kwa Mourinho!.

Ronaldo anafanya madhambi pale, haaa! mbaya sana ile, dhahiri shahiri mwamuzi atatoa adhabu, nini? eeeh! kadi nyekundu!

Hivyo ndivyo usiku huu watangazaji wa soka walivyotangaza wakati Real Madrid wakipoteza mchezo wa fainali wa Copa Del Rey dhidi ya Atletico Madrid huku Ronaldo na Mourinho wakioneshwa kadi nyekundu.

Kazi kwisha, kocha mwenye ngebe nyingi na maneno mengi zaidi duniani, Mreno Mario Jose Dos Santos Ferlix Mourinho hatimaye amemaliza msimu wa 2012/2013 bila kikombe chochote baada ya usiku huu kupoteza mchezo wa fainali ya Copa Del Rey kwa kufungwa mabao 2-1 na wapinzani wake wakubwa katika mji wa Madrid, klabu ya Atletico Madrid.

Bao la dakika za majeruhi lililotiwa kambani na mchezaji wa Atletico  Joao Miranda limeipa ushindi wa 2-1 na kuacha machungu makubwa kwa benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki wa Real De Madrid ambao wamemaliza msimu bila taji lolote huku wapinzani wao wakubwa FC Barcelona wakiwa wameshatwaa ubingwa wa La Liga.
Katika mchezo huo, dunia imeshangazwa na kitendo cha Kocha Mourinho kupewa kadi nyekundu na mwamuzi Clos Gomez kufuatia kutoelewana lugha , huku baadaye nyota wa klabu hiyo Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo naye akioneshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mchezaji Gab.


Wizara ya Maliasili na Utalii imeanza mikutano ya mchakato wa kupokea maoni kutoka kwa watu na makundi mbalimbali kuhusu uanzishwaji wa Mamlaka ya Wanyamapori (TAWA).
Mkutano wa kwanza umefanyika ljana Dar es Salaam katika Ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kampasi ya Bustani kwa kuanza kupokea maoni kutoka kwa viongozi waliowahi kuwa mawaziri,makatibu wakuu na wakurugenzi wa wizara kuhusu uanzishwaji wa Mamlaka hiyo.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki wakati akifungua mkutano huo alisema Sheria ya Wanyamapori ya Mwaka 2009 inaitaka Wizara kuanzisha Mamlaka ya Wanyamapori kazi ambayo itakamilika Novemba mwaka huu.

Mhe. Waziri alisema kuwa Wizara kwa kutambua umuhimu wa ushirikishwaji imeamua kuanza na viongozi waliowahi kuitumikia Wizara ili waweze kutoa maoni juu ya Sheria na Muundo wa Mamlaka ya Wanyamapori pamoja na Sheria ya Idara ya wanyamapori itakayobaki katika Wizara.
“Nyalaka hizi zimetengenezwa na watu wa ndani ya Wizara wenye uzoefu wa muda mrefu na hivyo tumeona ni vizuri tuwashirikishe ninyi viongozi mliowahi kuitumikia Wizara ili muweze kutoa michango yenu itakayotuwezesha kupata kitu bora kitakachopelekwa katika Baraza la Mawaziri na kisha kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ili Bunge la Novemba tuweze kuiwakilisha ikiwa ina baraka na maoni kutoka kwa kamati ya Bunge ili ipitishwe kama Sheria ya Mamlaka ya Wanyamapori,” alisema Mhe. Waziri.
Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Wanyamapori kutasaidia katika kurahisisha usimamizi wa rasilimali watu, kujitegemea kimaamuzi, na kuwa na uwezo wakujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha kutoka hadhina.
Miongoni mwa mawaziri waliohudhuria mchakato huo ni Mhe. George Kahama, Mhe. Getruda Mongella,  Mhe. Ezekiel Maige, Mhe. Dkt. Juma Ngasongwa, Mhe. Zabehi Mhita na Mhe. Arcado Ntegazwa.
Makatibu wakuu waliofika ni Mhe. Philimon Luhanjo, Mhe. Marten Rumbanga, Mhe. Rose Lugembe, Mhe. Balozi Dkt. Ladislaus Komba, Mhe. Alhaj Muhidin Ndolanga, Mhe. Salehe Pamba na waliowahi kuwa wakurugenzi wa Idara ya Wanyamapori. Chanzo: Tulizo Kilaga

No comments:

Post a Comment