Hii ni sehemu ya mwili iliyosalia kama inavyoonekana
Mabaki ya mwili huo yakiwa eneo la tukio kama yanavyoonekana
Askari kanzu wakiuchukua mwili huo baada ya kukutwa porini
Baadhi ya nguo alizokuwa nazo marehemu huyo ambae jina halijafahamika
Hiki ni kitenge ambacho alikuwa amevaa mwanamke huyo
Mashuhuda wa tukio hilo na askari kanzu wakitoka kuchukua mabaki ya mwili huo
Mabaki ya mwili wa mwanamke huyo yakihifadhiwa katika mfuko maaalum
Wananchi na polisi wakiupakia mwili huo katika gari la polisi mchana huu
Polisi wakiuhifadhi mabaki ya mwili huo chumba cha maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iring.
Toka kwa http://www.matukiodaima.com/
Mabaki ya mwili wa mwanamke mmoja
ambae anakadiliwa kuwa na miaka kati ya 25 hadi 30 imekutwa eneo la
Magereza Kata ya Miyomboni Kitanzini katika Manispaa ya Iringa leo.
Mabaki hayo yamekutwa majira ya saa 6
mchana wa leo ikiwa imesambaratika kutokana na kuoza imekutwa leo na
maofisa wa magereza ambao walikuwa katika eneo hilo na wafungwa
wakikata miti kwa ajili ya kuni na kukutana na mifupa hiyo.
Wakizungumza na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com
baadhi ya mashuhuda walidai kuwa mwanamke huyo ambae alikuwa
amevalia suruali nyeusi ,kilemba cha kitenge chenye madoa
makundu,njano ,meusi na meupe pamoja na skafu yenye rangi nyeupe na
nyeusi huku pembeni kukikutwa kitenge chake chenye rangi mchanganyiko
kama kilemba kwa maana ya makundu,njano ,meusi na meupe .
Hata hivyo mashuhuda hao walisema
kuwa mwanamke huyo alipoteza maisha yake kwa zaidi ya wiki mbili
kutokana na jinsi ulivyoharibika na kukauka kupita kiasi .
Mazingira ya kifo cha mwanamke huyo
yanaonyesha kuwa ni tata kutokana na polisi waliofika eneo hilo
kukiri kutokuwepo kwa taarifa yoyote ya mtu kupotea na kuwa
yawezekana alivamiwa ama alikufa kwa matatizo yake ama alikuwa akitoka
Hospitali
Hata hivyo eneo hilo ambalo mabaki
hayo ya mwili yamekutwa ni eneo ambalo lipo jirani zaidi na njia ya
mkato inayotokea Ipogolo hivyo ilikuwa ni rahisi zaidi watu kuuona
mwili huo.
Mabaki ya mwili huo yamechukuliwa na polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
No comments:
Post a Comment