FESTO SANGA BLOG:
TAARIFA za awali zina arifu kuwa Mfanya Biashara, Costa Shirima
anaedaiwa kujirusha kutoka gorofa ya tisa ya Hoteli ya Concord iliyopo
Kariakoo Jijini Dar es Salaam inaelezwa kuwa alikuwa asafiri na ndege
ya saa 10 jioni kuelekea China kufuata bidhaa za maduka yake.
Shirima (47), ambaye amefikwa na umauti muda mfupi baada ya kudondoka
chini ni mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki maduka kadhaa ya urembo wa
akina mama yaliyopo jirani na Hoteli hiyo ya Concord.
Aidha taarifa hizo za awali kutoka kwa mmoja wa wanafamilia ambaye
alidai kuwa si msemaji wa familia ya Shirima ya Mwika Moshi mkoani
Kilimanjaro, nikuwa Marehemu mara kwamara alikuwa akipendelea kula
katika hoteli hiyo na siku ya tukio inadaiwa kuwa aliwaeleza watu kuwa
anapanda juu ya Hoteli hiyo kupunga upepo baada ya kuhisi hewa nzito
mahali alipokuwa.
Inadaiwa kuwa baada ya kupanda huko juu ghafla alianguka chini na
kudondokea gari dogo aina ya Toyota Corola linalofanya biashara ya Taxi
na kupoteza maisha yake na gari hilo kuharibika vibaya kutokana na
kishindo hicho.
Marehemu Shirima mbali na kuwa Mfanya Biashara wa muda mrefu Kariakoo
pia alikuwa akiendelea na Ujenzi wa Jengo la Gorofa maeneo ya Kariakoo.
Marehemu ameacha mjane na watoto 5.
Uchunguzi wa Kipolisi bado unaendelea kuhusiana na tukio hilo na taarifa kamili zitatolewa pindi zitakapo kamilika.
No comments:
Post a Comment