Tukio hilo liloloonekana kumkosesha amani PHD, liliibuka Jumapili iliyopita ndani ya Ukumbi wa Bilicanas, Posta, jijini Dar wakati staa huyo alipokuwa akizindua singo yake mpya inayofahamika kwa jina la Rest of My Life.
Chanzo makini kilichoomba hifadhi ya jina, kilimtonya paparazi wetu kuwa wakati staa huyo akipafomu jukwaani alishika pafyumu kama swaga za kunogesha shoo huku akiwapulizia baadhi ya mashabiki wake, haswa warembo.
...Timbwili likiendelea.
“Aliwapulizia pafyumu baadhi ya warembo akiwa jukwaani lakini kumbe
kitendo kile hakikumpendeza mdada mmoja hivi aliyeonekana kama ni
shombeshombe.“Sasa akaona isiwe tabu, akasubiri aliposhuka jukwaani, akamfuata nyuma ya jukwaa (back stage) na kuanza kumshika shati huku akihoji kwa nini alimpulizia pafyumu hiyo bila ridhaa yake,” kilisema chanzo hicho.
..Wadau wakijaribu kumtuliza dada huyo.
Wakati mwanadada huyo akiwa amemtaiti PHD, baadhi ya watu waliokuwa
karibu waliingilia kati na kumsihi dada huyo apunguze munkari, zoezi
ambalo lilichukua takriban robo saa.Hemed alifanikiwa kuchomoka kwenye himaya ya mlimbwende huyo na kumwacha akiendelea kumchimba biti.
Juhudi za kumpata Hemed juzi Jumanne ili aeleze kwa undani kilichompata hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana hewani.
No comments:
Post a Comment