Habari
zilizotufikia kutoka Mtwara zinaeleza kuwa kumeibuka vurugu ambazo
zimepelekea mabomu ya machozi na risasi za moto kutumika baada ya Bajeti
ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa bungeni na kueleza kuwa mradi wa
gesi Mtwara utatekelezwa bila kutaja faida za moja kwa moja
watakazozipata wananchi hao. Inadaiwa kuwa kwa sasa kauli mbiu ya
wananchi walio katika maeneo hayo ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la
peni". Inaelezwa kuwa kituo cha mafuta cha Total kimechomwa moto wakati
wa vurugu hizo. Katika kukabiliana na vurugu hizo, inadaiwa polisi
kutoka Masasi na Lindi wapo eneo hilo kuongeza nguvu. Taarifa zaidi
zitawajia hivi punde
No comments:
Post a Comment