Monday, April 29, 2013

MASHTAKA YA MH.LEMA

Quote By Mungi View Post
Tayari hakimu Joyce Msofe ameingia, mahakama imeanza. Anasimama Wakili Method Kimomogoro anajitambulisha.

Hakimu: Hili ni shauri jipya, naomba lisomwe kama inavyostahili.

Lema unashatkiwa kwa kosa moja kinyume na sheria, ulichochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu, na kumzomea mkuu wa mkoa kama ifuatavyo, uliwaambia wanafunzi kuwa mkuu wa mkoa hajui chuo cha uhasibu ilipo, na amekuja akiwa amechelewa, anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.
Quote By Mungi View Post
Lema amekana kosa, na mwendesha mashtaka amesema dhamana lipo wazi kama atatimiza masharti ya dhamana. Taratibu za dhamana ndo inaanza sasa. Kesi itapangiwa tarehe nyingine pending investigation.
Quote By Mungi View Post
Kesi imeahirishwa mpaka tarehe May 29.

toka JF

No comments:

Post a Comment