Tuesday, April 30, 2013

BARCA, MADRID KITANZINI

Madrid, Hispania. Upinzani wa Barcelona na Real Madrid umepoteza heshima yake baada ya kupokea kipigo kizito katika mechi za kwanza za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na sasa wanahitaji miujiza kusonga mbele.Barcelona ambao walikubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Bayern Munich watakuwa wakijiuliza Jumatano katika mechi ya marudiano, huku ndugu zao Madrid wenyewe watakuwa na afueni kidogo leo kwani katika mechi ya kwanza walifungwa mabao 4-1 na Borussia Dortmund.
Hakuna timu iliyowahi kusonga mbele baada ya kufungwa idadi hiyo ya mabao katika hatua hii ya mashindano haya, hiyo ni ishara kuwa Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley inaweza kuwa fainali ya Wajerumani watupu.Kiwango kilichoonyeshwa na Dortmund na Munich za Bundesliga ya Ujerumani katika michezo ya kwanza, kimeifanya miamba hiyo Hispania, Barcelona na Madrid zinazosifika kwa kucheza soka la kushambulia kuwa shakani.Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amefunga mabao manane katika michuano hiyo.Naye nyota wa Madrid, Cristiano Ronaldo kwa sasa anaongoza kwa ufungaji akiwa amefunga mabao12, akifuatiwa na mshambuliaji wa Dortmund, Robert Lewandowski aliyefunga mabao 10, ambapo manne kati ya hayo alipachika dhidi ya Madrid wiki iliyopita.
Toka mwananchi.

No comments:

Post a Comment