Njemba moja,
Stephen Gough aliyewahi kuwa mwanajeshi amekamatwa na polisi katika Jiji
la Portsmouth, Uingereza baada ya kukutwa na mpenzi wake wakidunda
kutalii mitaani wakiwa uchi wa nyama.
Mwanamke Melodine Roberts
aliyefuatana naye aliachiwa na polisi kwa kuwa mara baada ya kuonywa
kuacha tabia hiyo, aliacha lakini mpenzi wake huyo aligoma na hii ni
mara ya 14 akifanya hivyo licha ya kufungwa jela huko nyuma
Baada ya
kugoma polisi walimfunga pingu na wakampeleka mahakamani moja kwa moja
ambapo Mwendesha Mashitaka, Simon Jones alisema Gough alikuwa amekiuka
sheria na aliwahi kufungwa miaka sita na moja ya makosa yaliyosababisha
afungwe ni kutemba uchi wa mnyama hadharani.
Baada ya maelezo
hayo, jaji aliyekuwa akisikiliza shauri hilo, Sarah Munro alisema kuwa
kwenda jela kwa mtu huyo ndiyo ilikuwa njia pekee kwake kwa kuwa hilo ni
kosa kubwa katika jamii ya Waingereza na ni ukiukwaji wa taratibu za
umma wa sehemu hiyo.
Gough alikiri kosa hilo na hakujitetea na jaji akamfunga miezi kumi na moja jela.
Source:Mpekuzi
No comments:
Post a Comment