Mwaka huu kazi ilikuwa moja kufanya plunning na kutengeneza fire line kuzuia moto kuingi ndani ya shamba, hii miti sasa ni mwaka wa 4 inaenda wa 5
Hapa nilijitutumua kupanda mwaka huu zaidi ya miche elfu 7 imewekwa hapo na nilitembelea inaendelea vizuri
Huu mche unakwenda vizuri miche y Viboringo haidanganyi ukisha ipanda inakuua tu wenyewe kikubwa kuzuia moto
Kwa mbali kule ni fire boundary ni moja ya sehemu niliyo panda mwaka huu zaidi ya ekali 10
Hii miti inakwenda vizuri baada ya mwaka jana kufanya plunning hapa sasa ina miaka 5 adui wa miti ni moto
Ile ile ya miaka 5 kwa mbali hapa naweza vuna ile gesi ya ukaye wanayo itangaza sana wenzetu
Hapa moto haukatishi kabisa labda ifanyike fitina vinginevyo moto utaishia pembeni
Kule juu vijana wamepanda mlima wote ule hakuna sehemu unaweza pata ukasema upande hata ekari mbili mwakani...
KILIMO CHA MITI.
Mi niliwahi panda miti enzi hizo nasoma Form II mwaka 1998 lakini baada ya miaka 9 ile miti alikuja kuivuna bibi yangu kibabe kwani ndiye aliyenipa shamba nipande miti nikipanda karibu ekari moja na ilikuwa mikubwa leo hii ningetangaza kuuza si chini ya Tsh.50,000/= kwa mti mmoja unao toa pingili 3 za futi 12 ubao, bibi yule aliuza miti yangu kwa bei ya kutupa kwa kila mti 15,000/= mpaka 20,000/= basi nikavunjika moyo kabisa swala zima la upandaji wa miti nikaamua kuacha. Hata hiyo ekari moja nilikuwa najaribu maana moto ulikuwa umekithiri sana maeneo ya Kipengere na viunga vyake uzuri niliipanda karibu na makazi ya watu hivyo basi moto ilikuwa ngumu kuingia.
Jamaa angu Abu Chaula ndiye aliye fufua matumaini yangu kuanza kufikiria tena kilimo cha miti nilihamasika wakati tunapiga story alipo nambia ana karibia ekari 40 za miti ya size tofauti tofauti, nikamuuliza anafanyaje fanyaje akanieleza baadhi ya maeneo alikuwa ananunua na bei zake zilikuwa kuanzia laki 2 mpaka 4 imezidi sana laki 6 au 7 kulingana na ukubwa wa miti, basi nami nikaamua kurudi rasmi kwa ajili ya kilimo hiki cha miti kama kijana naelewa na hadhina kwa baadae pindi uzee utakapo karibia. Kwa sasa kupata eneo la kupanda miti ni shughuli sana maana kila mtu anahamasika kupanda miti na maeneo ya kupanda yamekuwa yakipanda kila kukicha, serikali za kijiji zinauza ekari moja kwaTsh. 10,000/= kwa wananchi ila wananchi wao wanauza eneo kwa Tsh. 100,000/= kwa ekari na kupata hiyo ekari moja ni shughuri pevu maana waweza itafute na usiipate maana wanachi wenyewe ekari moja yenye miti ya umri wa miaka 3 wanauza mpaka milioni 1.2 wanaita ya kufuga.
No comments:
Post a Comment