CHADEMA | CCM |
Wapenzi wengi wa chama ni wananchi wa kawaida na masikini sana wanaotaka maisha yenye nafuu kidogo | Wapenzi wake wengi ni watu walioko kwenye system wanaopambana kuzilinda nafasi zao kwa njia yeyote ile. |
CHADEMA | CCM |
Chama na viongozi hulindwa na vijana dhoofu ili hali (wasiio na silaha yoyote) ila wenye za kichwani .Huifanya kazi hii kwa kushirikiana na wananchi wakawada. | Hulindwa na vyombo rasmi ikiwemo vyombo vya usalama vya serikali vyenye nyenzo za kisasa. |
VIONGOZI WAKE
CHADEMA | CCM |
Wanapenda kuchanganika na wananchi wa kawaida hata kama ni kwenye dala dala. | Wanapenda kuishi maisha ya juu na yakutukuzwa zaidi. |
Niwanyenyekevu Sana kwa wananchi | Wakati Fulani huwatisha wananchi hasa wanaofikiri kinyume na wao. |
KAMPENI
CHADEMA | CCM |
Wananchi huhudhuria mikutano kwa baahati nasibu tuu baada ya kutangaziwa. | Wahudhuriaji hukusanywa na kupelekwa kwa mabasi kwenye mkutano na kisha kupatiwa posho ya kujikimu. |
Wananchi ndio huwachangia wagombea ili waweze kufanya kampeni. | Wagombea ndio huwapa wananchi kitu kidogo ili waweze kuwachagua. |
Hueleza jinsi Serikali inayoongozwa na CCM, ilivyoshindwa kutekeleza majukumu yake. | Huilamu CHADEMA kwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi (japo wao ni wapinzani tu). |
KATIKA KUONGOZA SERIKALI
CHADEMA | CCM |
Ni Chama cha upinzani (ambacho sera zake haziwajibiki kutekelezwa)japo kwa kiwango kikubwa ndizo zinazotekelezwa.Mf; Mchakato wa katiba mpya | Ni Chama tawala (ambacho sera zake ndizo zinatakiwa zitekelezwe) ila wanapobanwa wanatekeleza za CHADEMA kwa kuwa hoja za CHADEMA zinakuwa nzito mno. |
BUNGENI
CHADEMA | CCM |
Wanapenda kuhoji mambo hata kama jambo linaonekana kuwa dogo. | Wana gonga meza hata msemaji anapotaja wilaya za Tanzania (mradi tu msemaji awe CCM). |
Wote Wako makini wakati wote. | Wengine wanasinzia, wanaongea, wanachat isipokuwa wachache tu ndio wanakuwa makini wakati wote. |
UWAZI
CHADEMA | CCM |
Ni wawazi sana na inapotokea jambo lenye utata kidogo tu wanakuja JF, au kuita vyombo vya habari kwa ajili ya ufafanuzi. | Ni wagumu wakutolea mambo ufafanuzi hadi waone hakuna tena ujanja .Wakati Fulani hata wakialikwa kwenye midahalo hawahudhurii. |
No comments:
Post a Comment