HAKUNA
maajabu hapa. Itakuwa fainali ya Wajerumani watupu Ligi ya Mabingwa
Ulaya Uwanja wa Wembley wiki tatu zijazo Jumamosi, ikiwakutanisha Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Hiyo inafuatia
Barcelona iliyomkosa Lionel Messi aliyekuwa benchi kutandikwa mabao 3-0
nyumbani usiku huu, baada ya awali kuchapwa 4-0 Ujerumani, hivyo
kutolewa kwa jumla ya mabao 7-0.
Barcelona
walionekana kabisa kuzidiwa uwezo na mapema tu walionekana hawawezi
kupanda mlima huo. Mabao ya Bayern ambao tayari ni mabingwa wa
Ujerumani, wakiivua taji Dortmund, yamefungwa na Arjen Robben dakika ya 49, Gerard Pique aliyejifunga dakika ya 72 na Thomas Muller dakika ya 76.
Kikosi cha Barca leo kilikuwa; Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra/Montoya dk87, Adriano, Xavi/Sanchez dk55, Song, Iniesta/Thiago dk64, Villa, Fabregas na Pedro.
Bayern Munich:
Neuer, Lahm/Rafinha dk77, Boateng, Van Buyten, Alaba, Javi
Martinez/Tymoschuk dk74, Schweinsteiger/Gustavo dk66, Robben, Muller,
Ribery na Mandzukic.
Wembley, tunakuja: Arjen Robben (katikati) akishangilia baada ya kufunga bao la kwanza Nou Camp
Fussball inakwenda nyumbani: Bayern imeungana na Wajerumani wenzao, Borussia Dortmund katika fainali
Hakuna kuzuia hiyo: Robben (haonekani) shuti lake likitinga nyavuni
Nyama za paja: Lionel Messi (kulia) alibaki benchi licha ya Barca kutakiwa kupiku kipigo cha mabao manne
Kichwa chini: Kipa wa Barca, Victor Valdes akilalamika baada ya Pique kujifunga
Kwisha habari yao: Thomas Muller wa Bayern akifunga bao la tatu
Wito wa London: Kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer (kushoto) na wachezaji wenzake wametinga fainali
Tatizo nini? Gerard Pique, David Villa na Cesc Fabregas wakitafakari kipigo
No comments:
Post a Comment