Madrid, Hispania. Upinzani wa Barcelona na Real Madrid umepoteza heshima
yake baada ya kupokea kipigo kizito katika mechi za kwanza za nusu
fainali ya Ligi ya Mabingwa na sasa wanahitaji miujiza kusonga mbele.Barcelona
ambao walikubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa Bayern Munich
watakuwa wakijiuliza Jumatano katika mechi ya marudiano, huku ndugu zao
Madrid wenyewe watakuwa na afueni kidogo leo kwani katika mechi ya
kwanza walifungwa mabao 4-1 na Borussia Dortmund.
Hakuna timu
iliyowahi kusonga mbele baada ya kufungwa idadi hiyo ya mabao katika
hatua hii ya mashindano haya, hiyo ni ishara kuwa Mei 25 kwenye Uwanja
wa Wembley inaweza kuwa fainali ya Wajerumani watupu.Kiwango
kilichoonyeshwa na Dortmund na Munich za Bundesliga ya Ujerumani katika
michezo ya kwanza, kimeifanya miamba hiyo Hispania, Barcelona na Madrid
zinazosifika kwa kucheza soka la kushambulia kuwa shakani.Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi amefunga mabao manane katika michuano hiyo.Naye
nyota wa Madrid, Cristiano Ronaldo kwa sasa anaongoza kwa ufungaji
akiwa amefunga mabao12, akifuatiwa na mshambuliaji wa Dortmund, Robert
Lewandowski aliyefunga mabao 10, ambapo manne kati ya hayo alipachika
dhidi ya Madrid wiki iliyopita.
Toka mwananchi.
No comments:
Post a Comment