Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.…
Rukia Haruna (31) akitolewa nje ya mahakama na askari kwenda gerezani kutumikia kifungo cha miaka mitano.
Pichani
juu ni taswira za wananchi wa eneo la Manga A jijini Mbeya wakati
wakijaribu kuokoa maisha ya kichanga kilichotupwa chooni na Rukia
Haruna Juni 14 mwaka huu.
Mwanamke Rukia Haruna (31), mkazi wa Manga A
Jijini Mbeya, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kosa la
kutupa mtoto wake chooni.
Tukio hilo lilitokea Juni 14, mwaka huu
katika eneo hilo baada ya watoto waliokuwa wakicheza kugundua kuwepo kwa
mtoto katika choo cha shimo.
Mtuhumiwa baada ya kukamatwa amekiri kutenda kosa hilo na kwamba alifanya hivyo baada ya mzazi mwenzie kumkataa.
Ameongeza kuwa alilazimika kutupa kichanga hicho katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Ameongeza kuwa alilazimika kutupa kichanga hicho katika choo cha jirani kwa sababu ni cha shimo tofauti na chao ambacho asingeweza kutupa mtoto huyo.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Archiles
Mulisa, mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, Zabibu Mpangula,
amemhukumu mtuhumiwa kifungo cha miaka mitano baada ya kosa hilo ambalo
ni kinyume cha kifungu 218 kifungu kidogo cha 35 sura ya 16 ya mwaka
2002.
HABARI NA MBEYA YETU BLOG
No comments:
Post a Comment